• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 6:09 PM
TUSIJE TUKASAHAU: Sharti waziri Zacharia Njeru asafishe Mamlaka ya Kitaifa ya Ujenzi

TUSIJE TUKASAHAU: Sharti waziri Zacharia Njeru asafishe Mamlaka ya Kitaifa ya Ujenzi

WATU kadha wanahofiwa kuzikwa kwenye vifusi vya jengo moja la orofa saba lililoporomoka katika eneo la Kasarani, Kaunti ya Nairobi jana Jumanne.

Visa vya majumba yanayojengwa kuporomoka na kusababisha maafa na majeruhi vimekithiri sehemu mbalimbali nchini licha ya kuwepo kwa asasi za kukagua ujenzi wa nyumba kuhakikisha ni salama.

Ikumbukwe kwamba mnamo Novemba 16, 2016 aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi, Miundomsingi, Nyumba na Ustawi wa Miji James Macharia, alitaja ufisadi katika Mamlaka ya Kitaifa ya Ujenzi (NCA) ndio chimbuko la mikasa kama hiyo.

Bw Macharia aliahidi kuwachukulia hatua kali maafisa wa NCA ambao alidai huhongwa na wamiliki wa majengo hayo ili wasiyakague kuhakikisha sheria zimezingatiwa katika ujenzi wayo.

Lakini zaidi ya miaka minne baadaye hamna afisa hata mmoja wa NCA, au asasi nyingine husika na ukaguzi wa majengo, ameadhibiwa kwa namna yoyote kuhusiana na uovu huo.

Kwa hivyo, Waziri Mpya wa Ardhi, Nyumba na Ustawi wa Miji Zacharia Njeru, akumbuke kuwa anakabiliwa na kibarua cha kushughulikia uozo katika NCA unaochangia kuporomoka kwa majengo.

  • Tags

You can share this post!

US kutoa Sh1.2b kunasa wakuu wa Al-Shabaab

CECIL ODONGO: Kupitia EALA wana wa Raila, Kalonzo wataiva...

T L