• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:57 PM
TUSIJE TUKASAHAU: Ulegevu wa maafisa wa NTSA na polisi wa trafiki unasababisha ongezeko la idadi ya vifo barabarani

TUSIJE TUKASAHAU: Ulegevu wa maafisa wa NTSA na polisi wa trafiki unasababisha ongezeko la idadi ya vifo barabarani

KULINGANA na takwimu zilizotolewa na Mamlaka ya Kitaifa ya Usalama Barabarani (NTSA), Januari 4, 2022 jumla ya watu 3,900 walikufa katika ajali za barabarani nchini kufikia Novemba 16, 2021.

Hii ni tofauti na watu 3,200 walioangamia ajalini wakati kama huo mwaka 2020.

Lakini mamlaka hiyo isije ikasahau kuwa hali hiyo inachangiwa na ulegevu miongoni mwa maafisa wake, na maafisa wa trafiki, katika kuhakikisha kuwa magari ya abiria yanazingatia sheria za usalama.

Kwa mfano, uchunguzi wa safu hii umebaini kuwa siku hizi ni nadra kwa abiria wanaosafiri kwa mabasi na matatu kujifunga mikanda ya usalama, kwa sababu mengi ya magari hayajawekwa mikanda hiyo.

Hii ndio maana magari haya yanapohusika katika ajali abiria wengi hufariki dunia.

  • Tags

You can share this post!

Haaland aongoza Dortmund kuponda Freiburg katika gozi la...

Omicron yafifia bara Afrika – WHO yasema

T L