• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 10:08 PM
Haaland aongoza Dortmund kuponda Freiburg katika gozi la Bundesliga

Haaland aongoza Dortmund kuponda Freiburg katika gozi la Bundesliga

Na MASHIRIKA

ERLING Braut Haaland alifunga mabao mawili na kusaidia waajiri wake Borussia Dortmund kuzamisha nambari nne SC Freiburg 5-1 katika mechi ya Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga).

Ushindi huo uliwezesha Dortmund wanaokamata nafasi ya pili kwenye msimamo wa jedwali la Bundesliga kupunguza pengo la alama kati yao na viongozi Bayern Munich hadi pointi tatu pekee.

Haaland ambaye ni fowadi raia wa Norway mwenye umri wa miaka 21 alifunga bao la tatu na la nne kwa upande wa Dortmund. Kufikia sasa, amepachika wavuni mabao 78 kutokana na mechi 77 akivalia jezi za Dortmund.

Thomas Meunier aliwaweka wenyeji Dortmund kifua mbele mwanzoni mwa kipindi cha kwanza kwa kupachika wavuni mabao mawili ya haraka.

Ingawa Ermedin Demirovic alifungia Freiburg na kufanya mambo kuwa 3-1, Mahmoud Dahoud aliongoza Dortmund kuzamisha kabisa chombo cha wageni wao mwishoni mwa kipindi cha pili.

Haaland sasa anajivunia rekodi ya kufungia Dortmund mabao 55 kutokana na mechi 56 za Bundesliga.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Wagonjwa wa kansa taabani mashini za KNH zikipata hitilafu

TUSIJE TUKASAHAU: Ulegevu wa maafisa wa NTSA na polisi wa...

T L