• Nairobi
  • Last Updated May 10th, 2024 1:50 PM
TUSIJE TUKASAHAU: Wakenya walioko katika kambi za IDPs wadi ya Salama wanahangaika sana

TUSIJE TUKASAHAU: Wakenya walioko katika kambi za IDPs wadi ya Salama wanahangaika sana

MNAMO Agosti 5, 2019 wakati wa mazishi ya aliyekuwa Gavana wa Bomet Joyce Laboso Rais Uhuru Kenyatta aliahidi kuwa serikali yake itakamilisha mpango wa kufidia wakimbizi wa ndani kwa ndani (IDPs) walioachwa nje katika mpango uliopita.

Lakini inaonekana kuwa serikali ya Rais Kenyatta haijatimiza ahadi hii huku muhula wake wa pili na wa mwisho uongozini ukielekea kukamilika.

Kwa mfano wakati huu, zaidi ya familia 1,500 za IDPs hao ambao ni waathiriwa wa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa 2007, bado wanaishi katika mazingira duni katika wadi ya Salama, eneobunge la Laikipia Magharibi, kaunti ya Laikipia.

Wengi wa watoto wao hawaendi shuleni kutokana na ukosefu wa nafasi na walimu wa kutosha katika shule ya msingi ya Kianjogu, iliyoko karibu na eneo ambako wanaishi katika mabanda.

You can share this post!

Wakazi wanung’unika baada ya Ruto kuteua mwaniaji kiti...

Urusi yalipiza kwa vikwazo vya Biden

T L