• Nairobi
  • Last Updated May 10th, 2024 6:43 AM
TUSIJE TUKASAHAU: Yusuf Hassan aishinikize serikali itekeleze mapendekezo ya kubuni BAKIKE

TUSIJE TUKASAHAU: Yusuf Hassan aishinikize serikali itekeleze mapendekezo ya kubuni BAKIKE

MNAMO Jumatano, Bunge la Kitaifa lilipitisha hoja inayopendekeza kubuniwa kwa Baraza la Kiswahili la Kenya (BAKIKE) litakalopiga jeki mchakato wa ukuzaji na uendelezaji wa Kiswahili nchini.

Hoja hiyo, ambayo ilidhaminiwa na Mbunge wa Kamukunji Yusuf Hassan, pia inahimiza serikali kuu kupalilia ushirikiano kati ya vyombo vya kiserikali na kibinafsi kufanikisha ajenda hii.

Lakini Bw Hassan, na wabunge wengine, wasije wakasahau kuwa mnamo Mei 13, 2016, bunge la 11 lilipitisha hoja sawa na hiyo lakini likafeli kuisukuma serikali ibuni BAKIKE.

Hoja hiyo ilidhaminiwa na aliyekuwa Mbunge Mwakilishi wa Taita Taveta Joyce Lay katika kikao ambacho Bw Hassan mwenyewe alihudhuria na kutoa mchango wake.

Kwa hivyo, sasa ni wajibu wa Mbunge huyu wa Kamukunji kushinikiza serikali, kupitia kamati ya bunge kuhusu utekelezaji, itekeleze mapendekezo ya hoja hii.

You can share this post!

Njaa: Watu 8 milioni hatarini Sudan Kusini

Kichaa cha mbwa chavamia kaunti 8 nchini

T L