• Nairobi
  • Last Updated June 12th, 2024 4:24 PM
TUSIJE TUKASAHAU: Wakenya 8.8 milioni walemewa kulipa ada za michango yao NHIF

TUSIJE TUKASAHAU: Wakenya 8.8 milioni walemewa kulipa ada za michango yao NHIF

JUMLA ya Wakenya 8.8 milioni wamelemewa kulipa michango yao ya kila mwezi kwa Bima ya Kitaifa ya Afya (NHIF) kufikia Januari 2023, kulingana na asasi hiyo.

Hii ni tofauti na hali ilivyokuwa mwaka mmoja uliopita ambapo jumla ya Wakenya 5.03 milioni walikuwa wamelemewa kulipa ada za NHIF.

Imebainika kuwa umasikini ni sababu kuu inayochangia hali hii ya Wakenya kushindwa kulipia ada za bima ambayo ni kiungo muhimu katika upatikanaji wa huduma za afya.

Lakini ikumbukwe kwamba Rais William Ruto aliahidi kwamba kufikia Desemba 2022, serikali yake itahakikisha kila kila Mkenya anasajiliwa kwa Bima ya NHIF.

“Mungu akipenda, kufikia mwishoni mwa mwaka huu, 2022, Wakenya wote watakuwa na bima ya NHIF. Kwa wale ambao hawawezi kulipa ada ya kila mwezi ya Sh500 kwa bima hii, nitahakikisha kuwa serikali inawalipia. Chini ya uongozi wangu kama Rais wa Kenya kila Mkenya atakuwa akitibiwa na kuenda nyumbani na matibabu hayo yatagharimiwa na NHIF,” akasema mnamo Februari 10, 2022 alipokuwa akiendesha kampeni Nyamira.

  • Tags

You can share this post!

Jopo lashauri Ruto amtimue Jaji Chitembwe

Walioangamia kwenye tetemeko wafika 8,100

T L