• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 9:01 PM
WANDERI KAMAU: Wanasiasa wakuu nchini wana ‘deni’ kubwa la kulipa vijana 2022

WANDERI KAMAU: Wanasiasa wakuu nchini wana ‘deni’ kubwa la kulipa vijana 2022

Na WANDERI KAMAU

KATIKA historia ya Kenya, ahadi kwa vijana kwamba watakuwa “viongozi wa kesho” zilianza tangu uhuru.

Awali, kulikuwa na matumaini miongoni mwa vijana nchini, baada ya serikali ya Mzee Jomo Kenyatta kuwashirikisha baadhi ya viongozi barobaro kwenye uongozi wake kama vile Tom Mboya, Mwai Kibaki kati ya wengine.

Kwenye baraza lake la kwanza la mawaziri 1964, Mzee Kenyatta alimteua Bw Mboya kuwa Waziri wa Mipango ya Kiuchumi na Maendeleo.

Mabarobaro wengine kama Bw Kibaki, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu Charles Njonjo na marehemu Daniel Moi walipewa nyadhifa nyingine muhimu serikalini.

Hata hivyo, serikali iliwageuka vijana hao baadaye, hasa iwapo walionekana “kukaidi” baadhi ya matakwa ya uongozi uliokuwepo.

Hilo ndilo lilichangia Mboya kuuawa kikatili katika hali tatanishi 1969 akiwa na umri wa miaka 38 pekee.

Serikali ya Moi ilionekana kufuata mkondo wa Mzee Kenyatta kuwatenga na kuwahangaisha vijana.

Badala ya kuwalea na kuwakuza vijana, serikali hiyo iliwageuka na kuwadhulumu viongozi ambao nyota zao za kisiasa zilionekana kung’aa.

Hadaa hizo ndizo ziliwafanya vijana wengi kutojitokeza kujisajilisha kama wapigakura kwenye zoezi lililoendeshwa juzi na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).

Bila shaka, mwelekeo huo unafaa kuwafungua macho vigogo wanaowania urais mwaka 2022 kwamba, wana kibarua kutimiza ahadi zote wanazotoa kwa vijana.

[email protected]

  • Tags

You can share this post!

DOUGLAS MUTUA: Kuwaadhibu wakuu wa magereza ni...

Bayern Munich waduwazwa na Augsburg ligini

T L