• Nairobi
  • Last Updated December 5th, 2023 10:25 PM
Bayern Munich waduwazwa na Augsburg ligini

Bayern Munich waduwazwa na Augsburg ligini

Na MASHIRIKA

VIONGOZI wa Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga), Bayern Munich waliduwazwa na Augsburg kwa kichapo cha 2-1 mnamo Ijumaa usiku ugani Augsburg Arena.

Ushindi huo wa Augsburg uliwaondoa kwenye mduara wa vikosi vinavyokodolea macho hatari ya kuteremshwa ngazi kwenye Bundesliga mwishoni mwa msimu huu.

Licha ya Bayern kutamalaki mchezo na kumiliki asilimia kubwa ya mpira, Augsburg walijiweka kifua mbele kupitia mabao ya Mads Pedersen na Andre Hahn kabla ya kigogo Robert Lewandowski kusawazisha mambo katika dakika ya 38.

Kichapo ambacho Bayern walipokezwa kilitamatisha rekodi ya kutoshindwa kwao katika mechi nne mfululizo ligini.

“Augsburg walicheza vizuri na walistahili ushindi. Nimesikitika sana kwa mara ya kwanza nikiwa kocha wa Bayern. Tulipata nafasi nyingi za wazi ambazo hatukuzitumia ipasavyo katika kipindi cha kwanza. Tulipoteza mpira kirahisi licha ya kujivunia idadi nzuri ya viungo wa haiba kubwa,” akasema kocha Julian Nagelsmann.

Mechi hiyo ilikuwa ya 600 kwa kiungo mzoefu Thomas Muller kuchezea Bayern waliokosa huduma za wanasoka watatu walioko karantini, akiwemo kiungo matata raia wa Ujerumani, Joshua Kimmich.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

WANDERI KAMAU: Wanasiasa wakuu nchini wana...

Kaburi la Mekatilili sasa kugeuzwa ‘chuo’ cha utamaduni

T L