• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 7:55 AM
WANDERI KAMAU: CBC: Jopo litilie maanani kuwapunguzia wanafunzi mzigo wa masomo

WANDERI KAMAU: CBC: Jopo litilie maanani kuwapunguzia wanafunzi mzigo wa masomo

NA WANDERI KAMAU

KWENYE makala aliyoandika Jumamosi iliyopita katika gazeti moja, msomi na mchanganuzi Barrack Muluka alilalamika kuhusu hali, mwelekeo na kiwango cha elimu nchini Kenya.

Msomi huyo aliufananisha mfumo wa elimu nchini na “mzigo mkubwa” anaotwikwa mwanafunzi mchanga, ambaye kimsingi anafaa kupewa nafasi kuufurahia utoto wake.

Dkt Muluka, ambaye majuzi alimaliza kusomea shahada yake ya uzamifu katika Uhusiano wa Kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha Leicester nchini Uingereza, anasema kuwa huu ni wakati muhimu kwa Kenya kutathmini tena na kulainisha mfumo wake wa elimu.

Kwenye makala hayo, msomi huyo alisema kuwa ingawa Kenya inalenga kufananisha mfumo wa Elimu ya Umilisi na Utendaji (CBC) na mfumo sawa unaoendeshwa nchini Finland, bado kuna mapengo makubwa yaliyopo, ambayo yanafaa kuzingatiwa.

Kulingana naye, moja ya mapengo hayo ni mwanafunzi kulazimishwa kuamka mapema na kurejea nyumbani karibu nyakati za usiku kwa kisingizio cha kuhakikisha kuwa “ameelewa masomo vizuri”.

Bila shaka mwelekeo huo ndio umekuwa ukifuatwa katika utekelezaji wa mfumo wa 8-4-4, unaosisitiza matokeo ya wanafunzi katika mitihani, badala ya ujuzi na maarifa waliyopata kwenye masomo yao.

Ni bayana kuwa huku jopo maalum lililoteuliwa na Rais William Ruto likiendelea na mchakato wa kusikiliza maoni ya wananchi kuhusu ulainishaji wa mfumo wa elimu nchini, ni wakati mwafaka lizingatie njia na namna ya kuwapunguzia wanafunzi mzigo wa kimasomo waliotwikwakwa sasa.

  • Tags

You can share this post!

DOUGLAS MUTUA: Waombeeni wasanii wa injili waziepuke kashfa...

Kioevu cha kuosha vyombo nyumbani kina matumizi aina aina

T L