• Nairobi
  • Last Updated February 23rd, 2024 12:48 PM
WANDERI KAMAU: Je, kauli tata ya Seneta Cheruiyot ni sera mpya ya serikali ya Kenya Kwanza?

WANDERI KAMAU: Je, kauli tata ya Seneta Cheruiyot ni sera mpya ya serikali ya Kenya Kwanza?

NA WANDERI KAMAU

KATIKA mpangilio wa kiutawala uliopo nchini kwa sasa, Kiongozi wa Wengi katika Seneti ni mtu mwenye ushawishi sana.

Kimsingi, yeye, mwenzake kutoka Bunge la Kitaifa na maspika katika mabunge yote mawili – Bunge la Kitaifa na Seneti – ni watu walio na ukaribu mkubwa sana na Rais aliye mamlakani.

Hivyo, wakati mwingine matamshi yao huonyesha sera, msimamo na mwelekeo wa serikali kuhusu masuala tofauti.

Kulingana na Katiba, viongozi hao ni miongoni mwa wale wanaoweza kuchukua uongozi wa nchi katika hali ambapo Rais na Naibu Rais hawapo nchini, ama hawawezi kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwa sababu ya ugonjwa mahututi au kifo.

Katika hali hiyo, inadhihirika wao ni watu wenye ushawishi mkubwa kisiasa na kikatiba.

Urejeleo huu mfupi unafuatia ujumbe uliochapishwa na Kiongozi wa Wengi katika Seneti, Aaron Cheruiyot, katika mtandao wa Twitter siku ya Jumatatu.

Bw Cheruiyot alisema kwamba lazima Rais Ruto akabili sekta mbili kuu muhimu ili kupata udhibiti kamili wa nchi — benki na vyombo vya habari.
Seneta Cheruiyot alizitaja sekta hizo mbili kuwa maarufu na zenye ushawishi mkubwa, na hivyo itamhitaji Rais “kutumia nguvu zake ili kuzikabili”.

Bila shaka, kauli hii si jambo la kuchukuliwa kwa urahisi kutokana na nafasi muhimu anayoshikilia Bw Cheruiyot katika utawala wa Kenya Kwanza.

Sasa ni lazima maafisa wakuu serikalini — akiwemo Rais Ruto — wajitokeze na kutoa ufafanuzi kuhusu ikiwa hiyo ndiyo sera mpya ya serikali dhidi ya benki na vyombo vya habari au la.

Je, Seneta huyo aliropokwa tu bila kujali? Ni wakati serikali ifafanue, la sivyo tunaelekea pabaya kuliko hali ilivyokuwa chini ya utawala wa kiimla wa chama cha Kanu.

  • Tags

You can share this post!

Mfanyabiashara akana kuilaghai kampuni bidhaa za maziwa za...

Kipa wa Gaspo Women aomba msaada kutibu jeraha

T L