• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 9:48 PM
Kipa wa Gaspo Women aomba msaada kutibu jeraha

Kipa wa Gaspo Women aomba msaada kutibu jeraha

NA AREGE RUTH 

KIPA chaguo la kwanza wa Gaspo Women Pauline Kathuru, ambaye alipata jeraha alipokuwa akicheza dhidi ya Ulinzi Starlets katika mechi ya Ligi Kuu ya Wanawake nchini (KWPL) anaomba msaada kugharamia matibabu yake.

Mwenyekiti wa timu hiyo Edward Githua, akizungumza na Taifa Spoti amemshukuru Rais mstaafu Uhuru Kenyatta kwa kuchangia Sh100,000.

“Kipa wetu Pauline Kathuru anahitaji upasuaji maalum wa matibabu katika hospitali ya PCEA Kikuyu ili kuokoa maisha yake ya soka,” amesema Bw Githua.

Bili ya gharama zake za matibabu ni Sh161,000.

Mchezaji huyo wa Harambee Starlets na ambaye aliwahi kuichezea klabu ya YANGA Princess ya Tanzania, amekuwa wa msaada mkubwa kwa Gaspo msimu huu.

Kwa sasa ndio vinara wa ligi wakiwa na alama 24. Wameshinda mechi saba, wakapiga sare tatu na kupoteza mechi moja.

  • Tags

You can share this post!

WANDERI KAMAU: Je, kauli tata ya Seneta Cheruiyot ni sera...

Kazi mwitu: Ajenti ashtakiwa kwa kuwanyofoa watafuta ajira...

T L