• Nairobi
  • Last Updated February 26th, 2024 10:30 AM
WANDERI KAMAU: Magoha alionyesha umuhimu wa watu kubuni na kuzingatia misimamo yao

WANDERI KAMAU: Magoha alionyesha umuhimu wa watu kubuni na kuzingatia misimamo yao

NA WANDERI KAMAU

KIFO cha aliyekuwa Waziri wa Elimu, Profesa George Magoha, ni ishara ya wazi kuwa si lazima mtu ajiingize katika siasa ili kutoa mchango muhimu kwa nchi yake.

Profesa Magoha amesifiwa kote kote kutokana na juhudi alizoweka kuboresha sekta ya elimu.

Kwa kawaida, imani ya watu wengi barani Afrika ni kuwa, bila ya kujiingiza katika siasa, mtu hawezi kuwa maarufu au kuheshimika na jamii.

Hata hivyo, Prof Magoha amedhihirisha kuwa kwa kujituma na kujitolea katika jambo lolote lile, si lazima mtu awe siasani ili kuleta mabadiliko hayo.

Katika utendakazi wake wote, Prof Magoha aliepuka kuingiza siasa kazi yake.

Licha ya kuteuliwa na Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta, Prof Magoha daima alisisitiza kuwa lengo lake kuu ni kutoa huduma kwa mtoto wa Kenya—bila kujali anakotoka, jamii au tabaka lake.

Ijapokuwa kama mwanadamu, hakukosa kasoro zake, utendakazi wake wa kipekee ni mfano bora kwa kizazi cha sasa na vingine vijavyo kuwa ni muhimu kubuni na kuzingatia msimamo wako.

Kwa mfano, licha ya lawama nyingi alizoelekezwa kuhusu msimamo wake katika utekelezaji wa Mfumo wa Elimu ya Umilisi na Utendaji (CBC), msomi huyo hakukata kauli wala hakutishika—alisisitiza lazima mpango huo utekelezwe. Buriani, Prof.

  • Tags

You can share this post!

KCB wamwaga Sh5 milioni kwenye gofu ya wanawake ya Magical...

Delmonte: Wakazi wa Gatuanyaga wakerwa kwa kutohusishwa...

T L