• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 6:09 PM
WANDERI KAMAU: Wabunge chipukizi katika Bunge la 12 walivunja mioyo ya Wakenya wengi

WANDERI KAMAU: Wabunge chipukizi katika Bunge la 12 walivunja mioyo ya Wakenya wengi

NA WANDERI KAMAU

MNAMO Alhamisi, Spika wa Bunge la Kitaifa, Justin Muturi alitangaza kumalizika kwa kipindi cha Bunge la 12, baada ya kulivunja rasmi.

Hatua hiyo sasa inatoa fursa kwa wabunge kurejea katika maeneobunge yao kufanya kampeni katika juhudi za kuwarai wapigakura kuwachagua kwa mihula mingine.

Muhula huu unapomalizika, moja ya mambo yatakayokumbukwa kuhusu bunge hili ni uwepo wa idadi kubwa ya vijana na watu waliosoma sana.

Kwanza, hii ni hatua inayoonyesha kuwa, Kenya imepiga hatua kubwa katika kuwapa nafasi vijana na makundi yaliyotengwa kama wanawake nafasi zaidi za kisiasa.

Hata hivyo, kile kinashtua ni kuwa, licha ya uwepo wa idadi kubwa ya vijana, wanawake na watu waliosoma, Bunge hili halijapiga hatua kubwa kupitisha sheria au kuendesha mijadala muhimu ya kitaifa ikilinganishwa na mabunge ya hapo awali.

Bunge hili limeshuhudia mizaha mikubwa kutoka kwa wabunge, hali inayoibua wasiwasi kuhusu uzito ambao wabunge wanaochaguliwa nyakati hizi wanaochukulia majukumu yao.

Kwa mfano, vijana wengi waliochaguliwa ama kuteuliwa kama wabunge hawajatoa michango mikubwa ilivyotarajiwa baada yao kuingia bungeni mnamo 2017.

Kinaya ni kuwa, baadhi ya wabunge “wazee” ama waliohudumu kwa mihula kadhaa walionyesha utendakazi mzuri na wa kuridhisha ikilinganishwa na chipukizi hao.

Wengi wao walijitosa kwenye mivutano ya kisiasa na kikabila, badala ya kuwatetea vijana. Uchaguzi Mkuu wa Agosti unapokaribia, wito mkuu kwa wapigakura ni kuwachagua wabunge kulingana na utendakazi wao, wala si kwa misingi ya umri, dini, au jinsia yao.

  • Tags

You can share this post!

TZ yawarai viongozi wa upinzani walio uhamishoni warejee

Kithi, Mung’aro na Tinga wamenyana kwa mdahalo Kilifi

T L