• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 4:55 PM
WANTO WARUI: Kuna hatari serikali kujiondoa katika ufadhili wa vyuo vikuu vya umma

WANTO WARUI: Kuna hatari serikali kujiondoa katika ufadhili wa vyuo vikuu vya umma

NA WANTO WARUI

HIVI majuzi, Waziri wa Elimu, Ezekiel Machogu, alinukuliwa akisema serikali itasitisha ufadhili wake kwa vyuo vikuu vya umma nchini.

Suala hili limezua hali ya mshikemshike kwa sababu waziri alionekana kuropokwa bila kufanya mashauriano na yeyote. Washikadau wengi wamepinga vikali maoni hayo ya waziri huku wakisema kufanya hivyo ni kutumbukiza elimu ya vyuo vikuu katika lindi la maangamizi.

Ni kweli kuna hatari nyingi ambazo zinaweza kutokea ikiwa serikali itasitisha ufadhili wa vyuo vikuu. Kwanza, kuna utafiti ambao ni wa umuhimu mkubwa unaofanywa na vyuo vikuu.

Utafiti wa masomo yanayohusiana na utekelezaji wa kutafuta soko kama vile MB chB, uhandisi wa kilimo na uchumi unaotoka baharini ni baadhi tu ya miradi ambayo haiwezi kutekelezwa na vyuo vikuu bila ufadhili wa serikali kwa sababu miradi hii inahitaji pesa nyingi.

Isitoshe, vyuo vikuu havijaweza kuchukua idadi kubwa ya wanafunzi kama inavyohitajika kutokana na ukosefu wa miundomsingi kama vile makao na kumbi za kusomea.

Kutokana na hili, pesa ambazo vyuo vikuu vinakusanya kutoka kwa wanafunzi ni kiasi ambacho hakiwezi kusimamia mambo haya.

Ujenzi wa madarasa ya kusomea na kumbi za kutolea mihadhara umekumbwa na tatizo la uhaba wa fedha.

Aidha, kuna miradi mingi ambayo imeidhinishwa na usimamizi wa vyuo vikuu. Baadhi ya miradi hiyo imeanzishwa na mingine inasubiri kupokezwa pesa ili ianzishwe. Serikali ikijiondoa katika ufadhili ina maana kuwa miradi hii ya elimu itakwama au ididimie kabisa.

Tayari miradi mingi ya masomo katika vyuo vikuu vya umma inachukua muda mrefu kukamilishwa kuliko ilivyopangiwa kutokana na ukosefu wa pesa.

Vilevile, kuanzishwa kwa miundo bora ya elimu ya dijitali katika vyuo vikuu ni jambo halijawezekana kutokana na uhaba wa fedha.

  • Tags

You can share this post!

TAHARIRI: Wabunge wasitishe ulafi, wajali waathiriwa wa...

Majambazi kuona cha mtema kuni Nakuru

T L