• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 11:39 AM
WANTO WARUI: Wanafunzi wa Gredi ya Saba ni wa shule za upili, KNUT iwaachie KUPPET

WANTO WARUI: Wanafunzi wa Gredi ya Saba ni wa shule za upili, KNUT iwaachie KUPPET

Kulingana na chama cha KNUT, wanafunzi wa Gredi ya 7 bado ni wadogo kiumri kusomea katika mazingira sawa na wale wa kidato cha nne ambao umri wao ni mkubwa.

Kati ya changamoto zinazoweza kuwakumba wanafunzi hao ni pamoja na unyanyasaji, ubaguzi na msongo wa mawazo kwani watapitishwa katika mambo wasiyoweza kuyadhibiti na wenzao wenye umri mkubwa.

Hivi ni kweli kabisa kwani tofauti ya miaka kati ya mwanafunzi wa Gredi ya 7 na yule wa Kidato cha Nne ni kubwa mno.

Hata hivyo, itakuwa ni makosa kwa wanafunzi wa Gredi ya 7 kusomea katika mazingira sawa na wale wa shule ya msingi ilhali wanaitwa wanafunzi wa sekondari.

Kulingana na mtaala wa CBC, silabasi ya Gredi ya 7 inaelekeza wazi kuwa wanafunzi wa gredi hii wanasoma masomo ya sekondari.

Mahitaji ya kuwepo kwa lebu ni dhihirisho kuwa masomo ya Gredi ya 7 ni ya sekondari. Kutokana na jambo hilo, ni wazi kuwa KNUT haistahili kung’ang’ania wanafunzi hao wabaki katika shule za msingi kwa masomo yao ni ya sekondari.

Kwa upande mwingine, haitafaa kuwafunzia wanafunzi wa Gredi ya 7 katika sekondari zilizopo sasa. Hii ndiyo maana mtaala ulipendekeza kuwe na Sekondari za Daraja la Chini.

Bila shaka, sekondari hizo zinafaa kujisimamia kivyao. Mpango huu ndio ufaao bali si kuwaweka wanafunzi wa Gredi ya saba pamoja na wale wa Kidato cha Nne.

  • Tags

You can share this post!

Uhuru na Kagame watoa rai kwa M23

Ugali moto wa GMO wamchoma Ruto

T L