• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
Alexander-Arnold na Maguire kutochezea Uingereza dhidi ya Andorra na Hungary kwa sababu ya majeraha

Alexander-Arnold na Maguire kutochezea Uingereza dhidi ya Andorra na Hungary kwa sababu ya majeraha

Na MASHIRIKA

NAHODHA wa Manchester United, Harry Maguire, pamoja na beki matata wa Liverpool, Trent Alexander-Arnold, watakosa mechi zijazo za Uingereza za kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia za 2022 dhidi ya Andorra na Hungary mtawalia kwa sababu ya mejaraha.

Kwa mujibu wa kocha Ole Gunnar Solskjaer wa Man-United, beki Maguire anatarajiwa kusalia mkekani kwa wiki kadhaa zijazo kuuguza jeraha la mguu alilolipata dhidi ya Aston Villa katika mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) mnamo Septemba 25, 2021 ugani Old Trafford.

Nyota huyo wa zamani wa Leicester City pia hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachotegemewa na Man-United dhidi ya Villarreal katika gozi la Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) mnamo Septemba 29, 2021.

Kwa upande wake, Alexander-Arnold anauguza jeraha la kinena na alikosa mechi ya UEFA iliyokutanisha miamba hao na FC Porto ya Ureno mnamo Jumanne usiku.

“Ana tatizo la misuli kwenye kinena. Ni jeraha litakalomweka nje kwa muda na yasikitisha atakosa mechi kadhaa muhimu katika ngazi ya klabu na timu ya taifa,” akasema kocha Jurgen Klopp wa Liverpool kumhusu Alexander-Arnold.

Kocha Gareth Southgate wa Uingereza anatarajiwa kufichua kikosi atakachokitegemea katika vibarua vijavyo dhidi ya Andorra na Hungary mnamo Septemba 30, 2021.

Uingereza waliotinga fainali ya Euro 2020 na kuzidiwa ujanja na Italia, wameratibiwa kuvaana na Andorra ugenini mnamo Oktoba 9 kabla ya kuvaana na Hungary mnamo Oktoba 12 ugani Wembley.

  • Tags

You can share this post!

Uefa yakunja mkia kuadhibu Barcelona, Real Madrid na...

Italia na Argentina kuvaana kwenye mechi ya kuwania taji la...