• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:57 PM
Amerika yapepeta Mexico na kutwaa taji la Concacaf Gold Cup

Amerika yapepeta Mexico na kutwaa taji la Concacaf Gold Cup

Na MASHIRIKA

AMERIKA walipiga Mexico 1-0 katika muda wa ziada na kutia kapuni taji la soka ya Concacaf Gold Cup kwa mara ya saba katika historia.

Beki Miles Robinson wa Atlanta United alifunga bao la pekee na la ushindi katika mchuano huo uliochezewa jijini Las Vegas katika dakika ya 118. Goli hilo lilikuwa lake la tatu kimataifa ndani ya jezi za Amerika.

Ni mara ya kwanza kwa Amerika kutwaa ufalme wa soka ya Concacaf miongoni mwa mataifa ya Amerika Kaskazini, Amerika ya Kati na nchi za Caribbean tangu mwaka wa 2017.

Mexico ambayo ni timu ya pekee kuwahi kushinda taji hilo mara nyingi zaidi kuliko Amerika, ilianza fainali hiyo kwa matao ya juu japo ikapoteza nafasi kadhaa za wazi kupitia fowadi Rogelio Funes Mori aliyemtatiza pakubwa kipa Matt Turner wa Amerika.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Barshim na Tamberi wagawa dhahabu ya Olimpiki katika fani...

Arsenal kuvunja benki ili kusajili kiungo James Maddison