• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 9:16 PM
Argentina na Italia kuchezea gozi la Finalissima jijini London, Uingereza

Argentina na Italia kuchezea gozi la Finalissima jijini London, Uingereza

Na MASHIRIKA

MABINGWA wa soka ya bara Ulaya (Euro), Italia, watavaana na wafalme wa Copa America, Argentina katika gozi kali la Intercontinetal Cup mnamo Juni 1, 2022 jijini London, Uingereza.

Uwanja utakaokutumiwa kwa ajili ya mchuano huo almaarufu ‘Finalissima’ bado haujathibitishwa.

Mabingwa wa Euro na wafalme wa Copa America walikuwa wakikutana kila mwaka tangu 1960 kabla ya kivumbi hicho kuunganishwa na kuwa Fifa Club World Cup mnamo 2005.

Kubuniwa kwa kipute cha Finalissima ni mikakati ya kimakusudi kati ya Shirikisho la Soka la bara Ulaya (Uefa) na Shirikisho la Soka la Amerika Kaskazini na Kati (Conmebol) kufanya kazi kwa karibu na ushirikiano.

Mashirikisho hayo yalipinga hatua ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kubadilisha kalenda ya kandanda kimataifa ili kuandaa fainali za Kombe la Dunia kila baada ya miaka miwili.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Gretsa yatenga Sh100 milioni za upanuzi wa chuo

Aguero astaafu soka kwa sababu ya matatizo ya afya

T L