• Nairobi
  • Last Updated May 10th, 2024 6:24 PM
Aguero astaafu soka kwa sababu ya matatizo ya afya

Aguero astaafu soka kwa sababu ya matatizo ya afya

Na MASHIRIKA

SERGIO Aguero amesema anajivunia kipindi kizima ambacho amekuwa akitandaza soka kitaaluma na amekubali maamuzi magumu ya kustaafu ulingoni kwa ajili ya kulinda afya yake.

Aguero, 33, alishindwa kuzuia machozi kumtiririka alipotangaza kuangika daluga zake mnamo Jumatano, miezi sita pekee baada ya kuondoka Manchester City na kupata hifadhi mpya kambini mwa Barcelona.

Fowadi huyo raia wa Argentina alipelekwa hospitalini mnamo Oktoba 30, 2021 baada ya kupata matatizo ya kifua akichezea Alaves waliolazimishia Barcelona sare ya 1-1 katika Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga).

“Maamuzi ambayo nimefanya yamechochewa na haja ya kulinda afya yangu,” akasema Aguero.

Kocha Pep Guardiola wa Man-City alikuwa miongoni mwa watu waliohudhuria kikao kilichomshuhudia Aguero akitangaza kuangika rasmi daluga zake kwenye ulingo wa soka.

Hadi alipofikia maamuzi hayo ya kustaafu, Aguero alikuwa amefunga mabao 427 kutokana na mechi 786.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Argentina na Italia kuchezea gozi la Finalissima jijini...

GWIJI WA WIKI: Justina Syokau

T L