• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 6:55 AM
Arsenal yaendea AFC Bournemouth

Arsenal yaendea AFC Bournemouth

NA MASHIRIKA

LONDON, UINGEREZA

ARSENAL wanalenga kuandikisha ushindi wa tatu mfululizo watakapokutana na AFC Bournemouth katika pambano la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) leo usiku.

The Gunners wameanza msimu kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Crystal Palace na 4-2 dhidi ya Leicester City, huku Bournemouth wakianza kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Aston Villa kabla ya kuchapwa 4-0 na Manchester City.

Dhidi ya Aston Villa ya kocha Steven Gerrard, Bournemouth wanaonolewa na Scott Parker walionyesha kiwango cha juu, katika ushindi huo ambao mabao yalipatikana kupitia kwa Jefferson Lerma na Kieffer Moore.

Baada ya kucheza na Arsenal, Bournemouth maarufu kama The Cherries wataendelea kukabiliwa na mechi ngumu watakapoanza dhidi ya Liverpool kabla ya kuchafuana na Wolves, na baadaye kuonana na Norwich City katika pambano la EFL Cup juma lijalo.

Bournemouth wamefanikiwa kuwachapa Arsenal mara moja pekee mnamo 2018 walipowashinda 2-1 katika mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL), lakini waliwahi kutoka sare 1-1 walipokutana Disemba 2019 ugani Vitality Stadium.

Kikosi hicho cha Parker kilirejea kwenye ligi kuu baada ya kumaliza katika nafasi ya pili, nyuma ya Fulham kwenye Ligi ya Daraja la Pili maarufu kama Championship.

Kwa upande mwingine, Arsenal hawakumaliza miongoni mwa nne bora katika EPL, na badala yake walifunga msimu katika nafasi ya tano, kwa pointi mbili nyuma ya Tottenham Hotspur, ambapo watashiriki katika michuano ya Europa League msimu huu, badala ya ile ya Klabu Bingwa yenye hadhi ya juu.

The Gunners watakuwa wakikabiliana na timu iliyo na uwezo wa kufanya vyema msimu huu, licha ya kuanza msimu kwa matokeo ya kuridhisha.

Huenda kuwasili kwa Gabriel Jesus kumemaliza matatizo ya Arsenal kwenye safu ya ushambuliaji, baada ya staa huyo kufunga mabao mawili majuzi.

Licha ya ushindi mara mbili mfululizo, mashabiki hawajaridhika, hadi watakapoandikisha ushindi kadhaa, kabla ya kukutana na mahasimu wao Manchester United mapema mwezi ujao wa Septemba.

The Gunners, pamoja na mechi za maandalizi, wameshinda mechi nane mfululizo, matokeo yanayowafanya wengi kuamini kwamba wana uwezo mkubwa wa kushinda Bournemouth, leo usiku.

Ratiba ya mechi za leo Jumamosi ni: AFC Bournemouth v Arsenal, Tottenham Hotspur na Wolves, Crystal Palace na Astona Villa, Fulham na Brentford, Leicester City na Southampton, Everton na Nottingham Forest.

Kesho Jumapili: West Ham United na Brington & Hove Albion, Leeds United v Chelsea, Newcastle United na Manchester City, Manchester United na Liverpool.

  • Tags

You can share this post!

Welbeck sasa kuchezea Brighton hadi Juni 2024

NYOTA WA WIKI: Wilfried Zaha

T L