• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Aston Villa washiba sifa za kocha wao Unai Emery baada ya kupepeta Tottenham 2-0 katika EPL

Aston Villa washiba sifa za kocha wao Unai Emery baada ya kupepeta Tottenham 2-0 katika EPL

Na MASHIRIKA

KOCHA Unai Emery alikuwa mwingi wa sifa kwa masogora wake wa Aston Villa waliopokeza Tottenham Hotspur kichapo cha 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) ugenini.

Masihara ya kipa Hugo Lloris aliyekuwa akisakata mechi yake ya kwanza tangu mwisho wa fainali za Kombe la Dunia yaliruhusu Emiliano Buendia kuwaweka Villa kifua mbele katika dakika ya 50 kabla ya Douglas Luiz kufanya mambo kuwa 2-0 kunako dakika ya 73.

Villa wanaoshuhudia ufufuo mkubwa wa makali yao, sasa wameshinda mechi mbili mfululizo za EPL ugenini chini ya kocha Emery ambaye pia amewahi kudhibiti mikoba ya PSG, Arsenal, Valencia, Spartak Moscow, Sevilla na Villarreal.

“Nawashukuru sana wanasoka wangu kwa kujituma maradufu na kutoa ushindani uliostahili dhidi ya Spurs,” akasema Emery.

Spurs walioteremka kutoka ndani ya mduara wa nne-bora jedwalini, sasa wameshinda mechi zao mbili pekee kati ya saba zilizopita.

Ilitarajiwa kwamba mechi hiyo ingekutanisha tena makipa Lloris na Emiliano Martinez walioonyesha ubabe wao katikati ya michuma kwenye fainali ya Kombe la Dunia iliyoshuhudia Argentina wakifunga Ufaransa penalti 4-2. Hata hivyo, Martinez alisalia benchi.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO 

  • Tags

You can share this post!

TAHARIRI: Maafisa wapya wahakikishie raia usalama tosha

Chelsea wapoteza alama muhimu katika EPL baada ya kuambulia...

T L