• Nairobi
  • Last Updated May 11th, 2024 7:15 PM
Barcelona katika hatari ya kutofuzu 16-bora UEFA baada ya kukabwa koo na Benfica ugani Camp Nou

Barcelona katika hatari ya kutofuzu 16-bora UEFA baada ya kukabwa koo na Benfica ugani Camp Nou

Na MASHIRIKA

MATUMAINI ya Barcelona kutinga hatua ya 16-bora ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) yalididimizwa na Benfica ya Ureno iliyowalazimishia sare tasa katika mechi ya marudiano ugani Camp Nou mnamo Jumanne usiku.

Barcelona waliomiliki asilimia kubwa ya mpira walipoteza nafasi nyingi za wazi huku Yusuf Demir, 18, akipoteza akishuhudia kombora lake likibusu mwamba wa goli la Benfica. Mchuano wa mwisho wa Barcelona kundini ni dhidi ya viongozi Bayern Munich huku Benfica wakialika Dymano Kyiv ya Ukraine.

Barcelona ambao ni mabingwa mara tano wa UEFA watakuwa na ulazima wa kuangusha Bayern ili kufuzu iwapo Benfica watazamisha Dynamo katika mchuano huo wa Disemba 8, 2021. Japo wanajivunia rekodi ya kutoshindwa katika mechi tatu zilizopita kundini, Barcelona wamefaulu kufunga mabao mawili pekee kutokana na mechi tano zilizopita za UEFA.

Barcelona watashuka hadi Ligi ya Uropa iwapo Benfica watazamisha Dynamo nao washindwe kutamba Ujerumani. Kufikia sasa, Barcelona wanashikilia nafasi ya pili kwenye msimamo wa Kundi E kwa alama saba, mbili zaidi kuliko nambari tatu Benfica. Bayern wanaselelea kileleni mwa alama 15 huku Dynamo wakivuta mkia kwa pointi moja.

You can share this post!

Man-United wamvizia Valverde kuwa kocha mshikilizi...

Wanasoka walemavu kutoka Kenya kuenda Tanzania kushiriki...

T L