• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 9:35 PM
Wanasoka walemavu kutoka Kenya kuenda Tanzania kushiriki Kombe la Afrika

Wanasoka walemavu kutoka Kenya kuenda Tanzania kushiriki Kombe la Afrika

Na VICTOR OTIENO

TIMU ya taifa ya soka ya walemavu ya Kenya itaelekea nchini Tanzania hapo Alhamisi asubuhi kushiriki Kombe la Afrika (CANAF) jijini Dar es Salaam kutoka Novemba 25 hadi Desemba 5.

Vijana wa kocha Willis Odhiambo walifaa kusafiri mapema Jumatano. Haijabainika mara moja kwanini safari hiyo imesukumwa hadi Alhamisi. Kwenye dimba hilo, Kenya imekutanishwa na mabingwa wa dunia Angola na washindi wa Afrika Mashariki na Kati (Cecaaf) Rwanda katika Kundi B. Wanavisiwa wa Zanzibar pia wanapatikana katika kundi hili.

Wenyeji Tanzania pamoja na Morocco, Uganda, Sierra Leone, Liberia, Ethiopia, Gambia, Cameroon, Misri, Ghana na Nigeria pia wanashiriki mashindano haya ambayo timu nne za kwanza zitaingia Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Uturuki.

Kenya imeratibiwa kuanza kampeni yake dhidi ya Rwanda mnamo Jumamosi ugani Benjamin Mkapa kabla ya kupepetana na Zanzibar (Novemba 28) na Angola (Novemba 29). Mechi dhidi ya Rwanda inatarajiwa kuwa kali, hasa kwa sababu timu hizo zitakuwa zikifufua uhasama. Rwanda ilizaba Kenya 3-1 katika fainali ya Cecaafa mwaka 2019 nchini Tanzania.

“Wapinzani wetu wakuu ni Angola na Rwanda. Zanzibar si wakali sana, lakini hatuwadharau,” alisema Odhiambo na kufichua kuwa wanalenga kutwaa taji. Kenya ilishiriki Canaf kwa mara ya kwanza kabisa mwaka 2014 na kumaliza katika nafasi ya nne jijini Nairobi. Wakenya walikamata nafasi ya 12 mwaka 2014 na nambari tisa kwenye Kombe la Dunia 2014 na 2019 mtawalia.

You can share this post!

Barcelona katika hatari ya kutofuzu 16-bora UEFA baada ya...

Mukidza kuwa nahodha wa Kenya Simbas ikipepetana na...

T L