• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Barcelona na Espanyol nguvu sawa katika mechi ya La Liga iliyoshuhudia refa akichomoa kadi 16 za manjano na mbili nyekundu

Barcelona na Espanyol nguvu sawa katika mechi ya La Liga iliyoshuhudia refa akichomoa kadi 16 za manjano na mbili nyekundu

Na MASHIRIKA

BARCELONA walilazimishiwa sare ya 1-1 na Espanyol katika pambano la Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga) mnamo Jumamosi ugani Camp Nou.

Marcos Alonso aliwaweka Barcelona kifua mbele baada ya dakika saba za kipindi cha kwanza kabla ya Joselu Luis Mato kusawazisha mambo kupitia penalti ya dakika ya 73.

Hata hivyo, mchuano huo ulitawaliwa na hisia kali na ikashuhudia pande zote mbili zikikamilisha mchezo na wachezaji 10 pekee uwanjani. Beki Jordi Alba wa Barcelona alikuwa wa kwanza kufurushwa uwanjani baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya manjano katika dakika ya 78, sekunde 120 kabla ya Vinicius Souza naye kufurushwa ugani kwa kadi ya pili ya manjano baada ya kumkabili Robert Lewandowski visivyo.

Ingawa Leandro Cabrera wa Espanyol pia alifurushwa uwanjani kwa kadi nyekundu, maamuzi hayo ya refa yalibatilishwa na teknolojia ya VAR.

Licha ya kuambulia sare, Barcelona walirejea kileleni mwa jedwali la La Liga kwa wingi wa mabao ikizingatiwa kwamba wana alama 38 sawa na mabingwa watetezi Real Madria waliokung’uta Real Valladolid 2-0 mnamo Ijumaa usiku ugenini.

Refa Antonio Mateu Lahoz aliyefanya pia maamuzi mengi yenye utata wakati wa mechi ya Kombe la Dunia iliyokutanisha Argentina na Uholanzi kwenye hatua ya robo-fainali mwaka huu wa 2022 nchini Qatar, alichomoa jumla ya kadi 16 za manjano na mbili nyekundu katika pambano lililokutanisha Barcelona na Espanyol.

Pamoja na kadi 15 za manjano ambazo wachezaji walionyesha ugani, pia kocha wa Barcelona, Xavi Hernandez, alionyeshwa kadi ya manjano kwa kosa la kulalamikia baadhi ya maamuzi ya refa Lahoz uwanjani.

MATOKEO YA LA LIGA (Jumamosi):

Barcelona 1-1 Espanyol

Real Sociedad 2-0 Osasuna

Villarreal 2-1 Valencia

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Biashara ya miraa yanoga nchini Somalia uzalishaji...

Atwoli aunga mkono hatua ya Sakaja kuondoa matatu CBD...

T L