• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 6:55 AM
Biashara ya miraa yanoga nchini Somalia uzalishaji ukiongezeka Meru

Biashara ya miraa yanoga nchini Somalia uzalishaji ukiongezeka Meru

NA RICHARD MUNGUTI

KIWANGO cha miraa inayouzwa nchini Somalia kimeongezeka na kufikia tani 50 huku uzalishaji ukiongezeka Meru.

Kulingana na chama cha wanaokuza miraa cha Nyambene Miraa Trade Association (Nyamita), ongezeko la uzalishaji miraa limetokana na mvua iliyonyesha kwa wingi.

Pia utumiaji wa zao hili nchini Somalia umeongezeka katika miji mingine mbali na Mogadishu.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Nyamita Bw Kimathi Munjuri amelalama kwamba Serikali bado haijawaondoa mabroka wanaodai walipwe Sh550 kwa kilo moja ya Khat (miraa).

Hapo awali Kenya imekuwa ikipeleka tani 20 za miraa nchini Somali kwa siku.

Rais William Ruto aliahidi Septemba 2022 kwamba atawaondoa mabroka waliovamia biashara ya miraa na kudai walipwe marupurupu kabla ndege kuisafirisha hadi Mogadishu.

Bw Munjuri alisema ijapokuwa bei ya kununua miraa kutoka mashambani imepungua kutokana na kuongezeka kwa mauzo Somalia.

Lakini Bw Munjuri alifichua bei ya Khat inayotoka Kenya inanunuliwa sana kuliko ile ya Ethiopia.

“Mauzo ya Miraa kutoka Kenya imefikia tani 50 kwa siku. Miraa yetu tunauza kutokana na oda kutoka Somalia. Tunaomba serikali iingilie suala hili la uuzaji Khat Somalia tupate kuuza kwa bei ya juu,” alisema Bw Munjuri.

  • Tags

You can share this post!

PSG wapoteza mechi kwa mara ya kwanza tangu Machi 2022

Barcelona na Espanyol nguvu sawa katika mechi ya La Liga...

T L