• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 7:55 AM
Beki Mkenya Okumu amaliza ukame mkali wa magoli Ubelgiji

Beki Mkenya Okumu amaliza ukame mkali wa magoli Ubelgiji

Na GEOFFREY ANENE

BEKI Joseph Okumu alipata bao lake la kwanza baada ya michuano 38 na kusaidia KAA Gent kuzima KV Mechelen 1-0 kwenye Ligi Kuu ya Ubelgiji, Jumamosi usiku.

Mkenya huyo, ambaye goli lake la mwisho lilikuwa wakati Gent ilinyamazisha Belisia Bilzen 4-0 kwenye Belgian Cup mnamo Oktoba 27, 2021, alifuma wavuni mpira wa kichwa dakika ya 82 baada ya kukamilisha kona kutoka Sven Kums.

Bao hilo ni lake la kwanza kabisa akiwa KAA ligini tangu ajiunge nao kutoka Elfsborg nchini Uswidi mnamo Julai 2021.

Thamani ya Okumu imekuwa ikiongezeka. Aliwasili Gent akiwa na thamani ya Sh245.5 milioni, lakini sasa imepanda karibu maradufu, hadi Sh552.5 milioni.

Amesakata jumla ya michuano 46 msimu huu. Kwa sasa, Gent inawania tiketi ya kuingia mashindano ya ligi ya daraja ya tatu ya Bara Ulaya maarufu Europa Conference League dhidi ya Genk, Mechelen na Charleroi baada ya kukamilisha ligi nambari tano kwa alama 51. Lazima imalize juu ya mashindano hayo ya timu nne ili iingie Europa League Conference.

  • Tags

You can share this post!

Tim Wanyonyi sasa ndiye mwaniaji ubunge Westlands kwa...

Shirika latoa wito Wakenya wafuatilie kampeni za uchaguzi...

T L