• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 11:53 AM
Beki wa Kibera Black Stars FC asema klabu imejiwekea malengo ya kufuzu kushiriki FKF-PL

Beki wa Kibera Black Stars FC asema klabu imejiwekea malengo ya kufuzu kushiriki FKF-PL

Na JOHN KIMWERE 

BEKI wa Kibera Black Stars FC (KBS), Nicodemus Onyango anaamini kuwa wanatosha mboga kufanya kweli kwenye ngarambe ya Supa Ligi ya Taifa (NSL) na kutwaa tiketi ya kushiriki Ligi Kuu Kenya (FKF-PL) muhula ujao.

Mpiga gozi huyu  ambaye ni mara ya tatu anachezea timu hiyo amepania kuisadia kunasa tiketi ya kupandishwa ngazi kama alivyochochea FC Talanta kufuzu kushiriki Ligi Kuu Kenya.

”Tumeshiriki NSL kwa muda mrefu sasa ni vizuri nasi tujitume kiume kupigania nafasi ya kupanda ngazi,” anasema na kuongeza kuwa ana imani mchango wake utasaidia kikosi hicho.

Anashikilia kuwa baada ya kutazama kikosi hicho kwa  umakini amegundua wanakaa vizuri kumaliza kati ya nafasi mbili bora katika jedwali.

Anashauri wenzake kuwa wakaze buti buti kwenye mechi zao ili kutimiza azma yao maana muhula huu wameanza vyema. Difenda huyu aliyewahi kupigia wana benki wa KCB FC ya FKF-PL, msimu uliyopita alikuwa akisakatia FC Talanta.

KBS FC imeanza vizuri mbio za msimu huu ambapo katika msimamo wa kinyang’anyiro hicho imekamata nafasi ya pili kwa kuzoa alama 13, tatu mbele ya Naivas FC. Shabana FC inaongoza kwa kusajili pointi 19.

  • Tags

You can share this post!

AFYA: Jinsi unavyoweza kupunguza maumivu ya mgongo

Maswali yazuka kuhusu aliko ‘Sultani’ Joho

T L