• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 12:18 PM
Beki wa kuwapa mashabiki wasiwasi aitwa kikosini

Beki wa kuwapa mashabiki wasiwasi aitwa kikosini

Na MASHIRIKA

KOCHA Gareth Southgate wa timu ya taifa ya Uingereza amejumuisha wanasoka Jordan Henderson na Harry Maguire katika kikosi atakachokitegemea dhidi ya Ukraine na Scotland katika michuano ijayo ya kirafiki mnamo Septemba 2023.

Kiungo Henderson, 33, ametiwa katika kikosi cha Uingereza licha ya kuondoka Liverpool mnamo Julai 2023 na kuyoyomea Saudi Arabia kuvalia jezi za Al-Ettifaq.

Beki Maquire naye ameitwa kambini mwa Uingereza licha ya kutochezea waajiri wake Manchester United katika pambano lolote la msimu huu wa 2023-24.

Uingereza wamepangiwa kuvaana na Ukraine mnamo Septemba 9 nchini Poland katika mechi ya kufuzu kwa fainali za Euro 2024. Watamenyana baadaye na Scotland kirafiki mnamo Septemba 12, 2023.

Mechi dhidi ya Scotland ugani Hampden Park itakuwa ya 150 kati ya vikosi hivyo viwili.

Mvamizi wa Arsenal, Eddie Nketiah, na beki wa Chelsea, Levi Colwill, wameitwa kambini mwa Uingereza kwa mara ya kwanza pamoja na kiungo Kalvin Phillips ambaye hajawajibikia Manchester City katika pambano lolote kufikia sasa muhula huu.

Fowadi wa Chelsea, Raheem Sterling, hajajumuishwa katika kikosi cha Uingereza na hii ni mara ya tatu mfululizo kwa Southgate kumweka nje.

Tyrone Mings, Luke Shaw na John Stones wanauguza majeraha na nafasi zao zitatwaliwa na Ben Chilwell na Fikayo Tomori ambao wamerejeshwa kikosini.

Beki wa kulia wa Liverpool, Trent Alexander-Arnold, amejumuishwa miongoni mwa viungo watakaotegemewa na Uingereza baada ya kutamba awali katika nafasi hiyo katika mechi zilizoshuhudia kikosi chao kikipepeta Macedonia Kaskazini na Malta mnamo Juni 2023.

KIKOSI CHA UINGEREZA:

MAKIPA: Sam Johnstone (Crystal Palace), Jordan Pickford (Everton), Aaron Ramsdale (Arsenal).

MABEKI: Ben Chilwell (Chelsea), Levi Colwill (Chelsea), Lewis Dunk (Brighton & Hove Albion), Marc Guehi (Crystal Palace), Harry Maguire (Manchester United), Fikayo Tomori (AC Milan), Kieran Trippier (Newcastle United), Kyle Walker (Manchester City).

VIUNGO: Trent Alexander-Arnold (Liverpool), Jude Bellingham (Real Madrid), Conor Gallagher (Chelsea), Jordan Henderson (Al-Ettifaq), Kalvin Phillips (Manchester City), Declan Rice (Arsenal).

WAVAMIZI: Eberechi Eze (Crystal Palace), Phil Foden (Manchester City), Jack Grealish (Manchester City), Harry Kane (Bayern Munich), James Maddison (Tottenham), Eddie Nketiah (Arsenal), Marcus Rashford (Manchester United), Bukayo Saka (Arsenal), Callum Wilson (Newcastle United).

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Mwanamume afariki baada ya kuanguka kwa shimo la kina cha...

Newcastle United wana kibarua kigumu katika Kundi F

T L