• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:57 PM
Brighton waajiri kocha Roberto de Zerbi kujaza nafasi ya Graham Potter aliyeyoyomea Chelsea

Brighton waajiri kocha Roberto de Zerbi kujaza nafasi ya Graham Potter aliyeyoyomea Chelsea

Na MASHIRIKA

BRIGHTON wameteua kocha wa zamani wa Shakhtar Donetsk na Sassuolo, Roberto de Zerbi, 43, kudhibiti mikoba yao ya ukufunzi kwa kipindi cha miaka minne ijayo ugani Amex.

De Zerbi ambaye ni raia wa Italia, amekuwa bila kazi tangu Julai 2022 alipoagana na Shakhtar kutokana na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

De Zerbi alikuwa chaguo la kwanza la Brighton waliojipata katika ulazima wa kujaza pengo la Graham Potter aliyeyoyomea Chelsea kutwaa mikoba ambayo Mjerumani Thomas Tuchel alipokonywa ugani Stamford Bridge mwanzoni mwa Septemba 2022.

De Zerbi ambaye ni kiungo wa zamani wa Napoli, alitambisha Sassuolo sana kwa kipindi cha miaka mitatu akiwa kocha wao. Ameleta Brighton kikosi kizima cha wakufunzi waliokuwa wakishirikiana naye kambini mwa Shakhtar.

Kibarua chake cha kwanza kambini mwa Brighton ni pambano kali la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) dhidi ya Liverpool mnamo Oktoba 1, 2022 uwanjani Anfield.

De Zerbi anakuwa kocha wa tatu kuajiriwa na Brighton kwa mkataba wa kudumu tangu Sami Hyypia ajiuzulu mnamo 2014. Brighton ambao sasa wanakamata nafasi ya nne kwenye jedwali la EPL kwa alama 13, hawasakata mchuano wowote tangu waagane na Potter. Mechi zilizokuwa ziwakutanishe na Bournemouth na Crystal Palace ziliahirishwa baada ya kifo cha Malkia Elizabeth II.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

TALANTA: Gwiji wa zumari

Kaunti yaomba wenye biashara wasubiri kulipwa malimbikizo...

T L