• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 5:55 AM
Chelangat atetea taji la Mbio za Nyika za Kenya Police bila jasho jingi

Chelangat atetea taji la Mbio za Nyika za Kenya Police bila jasho jingi

Na CHRIS ADUNGO

SHEILA Chelangat aliongoza mbio za nyika za kilomita 10 za kitengo cha Huduma za Polisi kwa upande wa wanawake mnamo Januari 29 uwanjani Ngong Racecourse.

Mwanariadha huyo amekiri kwamba ushindi huo utampa jukwaa zuri la kutetea kwa mafanikio taji lake la kitaifa la Mbio za Nyika mnamo Februari 13 katika uwanja uo huo wa Ngong Racecourse.

“Najihisi vizuri baada ya kutamba katika mashindano yangu ya pili mwaka huu. Nia yangu katika kivumbi cha Ijumaa ilikuwa ni kuanza kwa matao ya juu nikiwa uongozini na kusubiri kuona iwapo yeyote angejitokeza kutoa ushindani,” akasema Chelangat aliyeibuka pia mshindi wa duru ya pili ya mbio za nyika za Shirikisho la Soka la Kenya (AK) mnamo Disemba 19 katika eneo la Mosoriot, Kaunti ya Nandi.

Mnamo Ijumaa, Chelangat alifika utepeni baada ya muda wa dakika 33:34.5 na kutawazwa mshindi kadri anavyojiandaa kwa mbio za RAK Half Marathon mnamo Februari 19 katika Falme za Kiarabu (UAE).

“Itakuwa baada ya kivumbi cha RAK Half Marathon ambapo nitaanza kushiriki mbio za masafa ya kadri ili kujiweka sawa na mashindano ya mita 5,000 kwenye Olimpiki za Tokyo, Japan mnamo Julai 2021,” akasema Chelangat.

Bingwa wa zamani wa dunia katika mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na vidimbwi vya maji, Hyvin Kiyeng aliambulia nafasi ya pili kwa muda wa dakika 33:39.5 mbele ya Edith Chelimo (33:40.5) na mshindi wa zamani wa nishani ya fedha katika mbio za mita 5,000, Margaret Chelimo (33:48.7).

You can share this post!

Gor Mahia wasajili fowadi matata Fonseca kutoka Brazil

Fowadi mahiri wa Galatasaray aingia katika sajili ya West...