• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 10:48 AM
Chipukizi wa Uingereza U-21 wapata kocha mpya

Chipukizi wa Uingereza U-21 wapata kocha mpya

Na MASHIRIKA

KIUNGO wa zamani wa Ireland, Lee Carsley, ameteuliwa kuwa kocha wa kikosi cha chipukizi wasiozidi umri wa miaka 21 nchini Uingereza.

Carsley anajaza pengo la Aidy Boothroyd aliyejiuzulu mnamo Aprili 2021 baada ya Uingereza kuvuta mkia katika hatua ya makundi kwenye kampeni za Euro.

Hiyo ilikuwa mara ya tano katika jumla ya mapambano sita ya haiba kubwa ambapo Uingereza U-21 walidenguliwa kwenye hatua ya makundi.

Carsley aliyewahi kuchezea Everton na Derby County, sasa atasaidiwa na mchezaji wa zamani wa Chelsea na timu ya taifa ya Uingereza, Ashley Cole.

Cole, 40, aliwahi kuvalia jezi za Uingereza mara 107. Mbali na kuwa msaidizi wa Carsley, ataendelea pia na majukumu yake ya sasa ya kuwatia makali wanasoka chipukizi katika akademia ya Chelsea.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Mzozo Tunisia wazidi kutokota Rais akimtimua waziri wa...

TENISI: Naomi Osaka aondolewa mapema kwenye Olimpiki 2020