• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 1:46 PM
Dinamo anayochezea Mkenya Onsando kuwania shaba Ligi Kuu ya raga Romania

Dinamo anayochezea Mkenya Onsando kuwania shaba Ligi Kuu ya raga Romania

Na GEOFFREY ANENE

KLABU ya CS Dinamo Bucuresti anayochezea Mkenya Malcolm Onsando imeaga vita vya kuwania taji la Ligi Kuu ya raga ya Romania.

Dinamo ilipoteza 32-15 dhidi ya mabingwa watetezi CSM Stiinta Baia Mare katika nusu-fainali ugani Zimbrilor Arena mnamo Oktoba 9.

Itamenyana na Timisoara katika mechi ya kuamua mshindi wa medali ya shaba nazo Baia na Steaua Bucuresti katika fainali mnamo Oktoba 16.

Mechi kati ya Baia na Dinamo ilishuhudia Dinamo ikichukua uongozi 7-5 kupitia mguso wa Marius Simionescu ulioandamana na mkwaju kutoka kwa Williams Jondre. Hii ni baada ya Baia kuongoza kupitia Florian Rosu.

Jondre alipoteza penalti tatu kabla ya Simionescu kutinga mguso wa kwanza. Ovidiu Cojocaru alirejesha Baia kifua mbele 10-7 kupitia mguso dakika ya 25. Hata hivyo, Dinamo ilisawazisha 10-10 Jondre alipopachika penalti. Cojocaru na Jason Tomane waliongeza miguso miwili ambayo Kisting alifanikiwa kufuma mikwaju yake na kuweka Baia 24-10 juu.

Johan Van Heerden alipunguza mwanya huo hadi 24-15 alipofungia Dinamo mguso bila mkwaju. Baia ilikamilisha ufungaji wake wa alama kupitia kwa Alexandru Alexe.

Dinamo walishinda ligi mara yao ya 16 na mwisho mwaka 2005.

Onsando, 25, ni mmoja wa wachezaji wanane kutoka ligi za kigeni ambao kocha Paul Odera anapanga kutumia mwezi Novemba wakati Kenya Simbas itashiriki mashindano ya mataifa manne dhidi ya Namibia, Brazil na Zimbabwe mjini Stellenbosch, Afrika Kusini.

Matokeo ya Dinamo Bucuresti ligini 2021:

Aprili 24 – CSA Steaua 38 CS Dinamo 36

Aprili 30 – CS Universitatea Cluj 30 CS Dinamo 52

Mei 8 – CS Dinamo 78 ACS Tomitanii Constanta 19

Mei 15 – CSM Stiinta Baia Mare 46 CS Dinamo 27

Mei 22 – CS Dinamo 31 CS SCM Timisoara 28

Mei 29 – CS Dinamo 14 CSA Steaua 27

Juni 6 – CS Dinamo 35 CS University of Cluj 20

Juni 12 – ACS Tomitanii Constanta 14 CS Dinamo 71

Septemba 5 – CS Dinamo 20 CSM Stiinta Baia Mare 22

Septemba 25 – CS SCM Timisoara 7 CS Dinamo 28

Oktoba 2 (robo-fainali) – CS Dinamo 63 ACS Tomitanii Constanta 17

Oktoba 9 (nusu-fainali) – CSM Stiinta Baia Mare 32 CS Dinamo 15

You can share this post!

Wizara yatoa onyo dhidi ya matumizi ya dawa ya kuua chawa

Ruto adai kumiliki kura za eneo la Mlima Kenya