• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 9:01 PM
Ecuador kushiriki Kombe la Dunia 2022 baada ya FIFA kufutilia mbali malalamishi ya Chile

Ecuador kushiriki Kombe la Dunia 2022 baada ya FIFA kufutilia mbali malalamishi ya Chile

Na MASHIRIKA

ECUADOR watanogesha Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar baada ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kufutilia mbali madai ya Chile kwamba waliwajibishwa mchezaji asiyestahili kwenye mechi za kufuzu kwa fainali hizo za Novemba-Disemba 2022.

Shirikisho la Soka la Chile (FFC) liliwasilisha malalamishi kwa FIFA kudai kuwa mwanasoka Bryon Castillo aliyechezea Ecuador mara nane kwenye mechi za kufuzu alikuwa raia wa Colombia na alidanganya kuhusu umri wake.

Hata hivyo, FIFA imeshikilia kuwa “baada ya kutathmini madai hayo kwa kina”, imeamua “kufunga kesi hiyo” dhidi ya Shirikisho la Soka la Ecuador.

Maamuzi ya FIFA yanamaanisha kwamba Ecuador watashiriki Kombe la Dunia wakiwa katika Kundi A linalojumuisha pia Senegal, Uholanzi na wenyeji Qatar.

Rais wa FFC, Pablo Milad, ameapa kukata rufaa dhidi ya FIFA katika Jopo Maalumu la Malalamishi ya Spoti (CAS).

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Mahakama yaelezwa jinsi mshukiwa alivyoiba simu akajaribu...

Uhispania wakomoa Czech na kutua kileleni mwa Kundi A2 la...

T L