• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 6:39 PM
Eric Johana Omondi ajiunga na klabu ya soka ya Muangthong United nchini Thailand

Eric Johana Omondi ajiunga na klabu ya soka ya Muangthong United nchini Thailand

NA GEOFFREY ANENE

MCHEZAJI wa kimataifa wa Harambee Stars, Eric Johana Omondi amejiunga na Muangthong inayoshiriki Ligi Kuu nchini Thailand kwa kandarasi ya mwaka mmoja Julai 22.

Kupitia mitandao ya kijamii, kiungo huyo mshambulizi amesema kuwa ni heshima kubwa malia ya klabu hiyo ambayo ni ya pili kwa kushinda Ligi Kuu mara nyingi baada ile ya Buriram United anayochezea winga Mkenya Ayub Timbe Masika.

“Nimekuwa nikifuata Muangthong United kwa muda sasa. Ni timu nzuri iliyo na makocha wazuri na mashabiki. Hii ni changamoto kubwa kwangu. Haikunichukua muda mrefu kuamua nataka kukuja hapa na kucheza… Natumai kuongoza timu kukamilisha mashindano katika nafasi nzuri na hata kunyakua mataji kadha katika msimu mpya,” alisema mchezaji huyo wa zamani wa Mathare United atakayevalia jezi nambari 19.

Kocha mkuu Mario Yurovsky alikaribisha Eric katika klabu ya Muangthong akisema, “Wewe ni mchezaji muhimu katika msimu utakaoanza mwezi Agosti. Mchezo wako wa kasi ya juu na kukamilisha mashambulizi bila shaka utatuongeza nguvu.”

Mabingwa wa Thailand mwaka 2009, 2010, 2012 na 2016 Muangthong watavaana na washindi wa 2006 True Bangkok United mnamo Julai 30 katika mechi ya kirafiki. Kabla ya kuelekea Thailand, Omondi, ambaye amechezea Kenya mara 25 tangu Oktoba 2015, alitandazia kabumbu Vasalund, Brommapojkarna na Jonkoping Sodra nchini Uswidi na Waasland-Beveren nchini Ubelgiji mtawalia. Waasland-Beveren ilimwachilia Julai 1.

  • Tags

You can share this post!

KASHESHE: Eti mtasubiri ndoa sana!

USIU yalenga kumaliza mashindano ikiwa miongoni mwa timu...

T L