• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 6:39 PM
USIU yalenga kumaliza mashindano ikiwa miongoni mwa timu Tano Bora Duniani 

USIU yalenga kumaliza mashindano ikiwa miongoni mwa timu Tano Bora Duniani 

Na JOHN KIMWERE 

TIMU ya wanawake ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha USIU ya mpira wa kikapu ni miongoni mwa vikosi vitakaoshiriki fainali za Kombe la Dunia (FISU) nchini Uchina mwaka 2023.

Maana hii ni timu ya shule wachezaji hawa wameichezea kwa kipindi cha miaka miwili baada ya wenzao kukamilisha elimu yao.

Warembo hao chini ya nahodha Yvonne Peace walijikatia tiketi ya kipute hicho baada ya kumaliza katika nafasi ya pili kwenye shindano la Vyuo Vikuu vya Afrika lililoandaliwa nchini Kenya mwezi Juni 2022.

USIU ya kocha George Mayienga iliibuka ya pili ilipozabwa kwa mabao 61-43 na America International University of Cairo (AIU) ya Misri  katika fainali.

”Licha ya kumaliza katika nafasi ya pili, tunafuraha tele kwa kuzingatia kwetu itakuwa mara ya kwanza kushiriki ngarambe hiyo itakayoleta pamoja timu kutoka kila bara kote duniani,” kocha huyo amesema na kuongeza wanajivunia kuwa watakuwa kati ya vikosi vitakaopeperusha bendera ya Kenya kwenye shindano hilo.

Kocha huyo anasema kampeni za ngarambe ya Afrika haikuwa mteremko kwani wapinzani wao kwenye fani zote walishusha upinzani wa kufa mtu.

Anashikilia kuwa wanatarajia ushindani mkali kutoka kwa washiriki wengine kutoka bara Ulaya wamepania kujituma kiume kwenye za kupigania kumaliza kati ya tano bora.

Baadhi ya wachezaji wa timu ya mpira wa kikapu ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha USIU (wenye nguo za mistari ya rangi ya manjano) wakikabiliana na wenzao. PICHA | JOHN KIMWERE

USIU imekuwa ikifanya vizuri kwenye ligi ya Vyuo Vikuu vya Kenya (KUSA) kanda ya Nairobi ambapo inajivunia kubeba taji hilo mara 12. ”Licha ya kushinda taji ndani ya kipindi hicho haijakuwa rahisi dhidi ya wapinzani wakuu nchini,” naibu kocha wa USIU, Peter Kajumbe anasema. Anataja wapinzani wakuu kama Chuo Kikuu cha Kenyatta (KU), Chuo Kikuu cha Strathmore na Chuo Kikuu cha Nairobi (UoN) kati ya nyingine.

Anatoa wito kwa viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu la Kenya (KBF) kuhakikisha wachezaji chipukizi wanapata nafasi kushiriki mechi za kitaifa ili kukuza talanta zao. ”Serikali inastahili kusapoti timu za taifa ili kusaidia wachezaji wetu kupaisha mchezo wao na kutambuliwa na mataifa mengine,” akasema.  Naibu anajivunia kuongoza wasichana hawa na kufanikiwa kubeba taji la KUSA mara moja ndani mwaka mmoja ambao wamekuwa nao.

USIU inajivunia kulea wachezaji zaidi ya kumi ambao huchezea klabu mbali mbali nchini.

Meneja wake, Tasha Mapenzi anashukuru menejimenti ya USIU kwa kufadhili vikosi vya mpira wa kikapu kati ya vingine kupalilia talanta zao.

”Kwa niaba ya timu ya kikapu ninashukuru viongozi wa chetu kwa kufahamu umuhimu wa kuwapa nafasi wanafunzi kuonyesha uwezo wao michezoni,” akasema.

USIU inajivunia wachezaji kama: Yvonne Peace (nahodha), Michelle Wacera, Frida Yagomba, Christine Omondi, Joan Menye, Neema Mollel, Aaliyah Havyarimana, Ann Waithera, Daniella Rehema, Vannessa Oluoch na Angelina Aluet.

  • Tags

You can share this post!

Eric Johana Omondi ajiunga na klabu ya soka ya Muangthong...

WANDERI KAMAU: Mdahalo wa urais uangazie sera...

T L