• Nairobi
  • Last Updated May 12th, 2024 3:24 PM
Everton wakomoa Palace na kukwepa shoka la kuwateremsha ngazi EPL

Everton wakomoa Palace na kukwepa shoka la kuwateremsha ngazi EPL

Na MASHIRIKA

EVERTON watasalia katika kampeni za Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) msimu ujao baada ya kutoka nyuma na kukomoa Crystal Palace 3-2 mnamo Alhamisi ugani Goodison Park.

Masogora hao wa kocha Frank Lampard walishuka dimbani wakifahamu kuwa kushindwa kungewateremsha ngazi hadi Ligi ya Daraja ya Kwanza (Championship) kwa mara ya kwanza baada ya miaka 68.

Hii ni baada ya Palace kufunga mabao mawili ya haraka kupitia kwa Jean-Philippe Mateta na Jordan Ayew kunako dakika ya 21 na 36 mtawalia.

Hata hivyo, Everton walirejea mchezoni dakika tisa baada ya mwanzo wa kipindi cha pili kupitia kwa goli la Michael Keane. Richarlison Andrade alipachika wavuni bao la pili la Everton katika dakika ya 75 kabla ya Dominic Calvert-Lewin kufunga la tatu. Bao la Calvert-Lewin ambaye amekuwa nje kwa muda mrefu msimu huu akiuguza jeraha lilikuwa lake la kwanza tangu Agosti 2021 dhidi ya Brentford.

Ushindi wa Everton ulirejesha kumbukumbu za 1998 na 1994 ambapo pia waliponea chupuchupu kushushwa daraja kwenye EPL. Kikosi hicho kitakachofunga kampeni za EPL msimu huu dhidi ya Arsenal mnamo Mei 22 ugani Emirates, sasa kinashikilia nafasi ya 16 kwa alama 39, nne zaidi kuliko Burnley na Leeds United. Palave wanakamata nafasi ya 13 kwa pointi 45 sawa na Aston Villa.

MATOKEO YA EPL (Alhamisi):

Everton 3-2 Palace

Aston Villa 1-1 Burnley

Chelsea 1-1 Leicester

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Vikao vya bunge vyaongezwa kwa wiki moja zaidi ili...

DCI yamsaka mshukiwa mkuu wa mauaji ya Samuel Mugoh Muvota

T L