• Nairobi
  • Last Updated June 12th, 2024 4:24 PM
FKF: Bandari yaikaribisha Vihiga United

FKF: Bandari yaikaribisha Vihiga United

Na ABDULRAHMAN SHERIFF

KUNA umuhimu wa kushinda mechi ya Ligi kuu ya FKF dhidi ya Vihiga United FC kwani ni kufanya hivyo tu ndiko kutaiweka timu katika nafasi nzuri kwenye ngazi ya ligi hiyo ambayo inaendelea kushuhudia matokeo mengine ya kushangaza.

Hayo yalikuwa matamshi ya Kocha Mkuu wa Bandari FC, Andre Cassa Mbungo aliyesema kuwa ana imani kubwa ya vijana wake kufanya vizuri na kupata ushindi kwenye mechi hiyo itakayopepetwa katika uwanja wa Mbaraki Sports Club, leo Jumanne Februari 23, 2021.

“Vijana wangu wako tayari kwa mchezo huu ambao tuna umuhimu nao wa kupata ushindi ili tuzidi kupanda ngazi na kuwa katika nafasi nzuri kwenye ngazi ya ligi. Tumefanya vizuri dhidi ya AFC Leopards na tunataka kuwashinda wapinzani wetu wa Vihiga,” akasema Mbungo.

Mkufunzi huyo alisema alifurahikia na jinsi wanasoka wake walivyocheza vizuri walipopambana na Leopards na haoni sababu ya kutofanya vizuri watakapojkutana uwanja wa nyumbani na Vihiga. Tunachotaka ni kupata pointi zote tatu,” akasema mkufunzi huyo.

Mkurugenzi wa Ufundi wa Cosmos FC, Aref Baghazally ametoa ombi kwa Mbungo awachezeshe wanasoka watatu ambao anaamini wanaweza kufanya vizuri wakipewa nafasi ya kuwa uwanjani kuiwakilisha timu hiyo.

Baghazally aliwataja Dennis Magige, Swaleh Chacha na Hassan Iddi kuwa chipukizi ambao wanaweza kucheza vizuri kutokana na kuwa na viwango vya hali ya juu vya kusakata soka.

“Nataka Mbungo awape fursa ya kucheza na nina uhakika watacheza vizuri,” akasema.

Baghazally amesema kuwaweka benchi ama kutowaweka kabisa kwa benchi kutawamaliza vijana hao ambao anaamini wanainukia vizuri na wanaweza kucheza vizuri kuisaidia Bandari kufanya vizuri ligini.

You can share this post!

Tuchel awataka Chelsea kujihadhari dhidi ya mfumaji Luis...

Kocha Flick ahimiza Bayern Munich watumie mechi ya leo ya...