• Nairobi
  • Last Updated June 12th, 2024 4:24 PM
Gaspo Women kuzuru TZ na Uganda kwa mechi za kirafiki

Gaspo Women kuzuru TZ na Uganda kwa mechi za kirafiki

NA TOTO AREGE

WAREMBO wa Gaspo Women ya Ligi Kuu ya Wanawake nchini Kenya (KWPL), watacheza mechi mbili za kirafiki nchini Tanzania na Uganda mtawalia.

Hili limefichuliwa saa chache tu baada ya aliyekuwa mchezaji wa zamani wa Harambee Stars Sammy Owino kuahidi kuwapa zawadi ya Sh500,000 kwa kumaliza wa pili nyuma ya mabingwa Vihiga Queens katika msimu uliokamilika wa 2022/23 KWPL.

Mwenyekiti wa klabu Edward Githua amesema kuwa kila kitu kiko sawa na hivyo wako tayari kucheza mechi hizo mbili.

“Tutatoa mpango wa kina baadaye lakini klabu zote zimethibitisha ziko tayari kutukaribisha,” akasema Bw Githua.

Gaspo kupitia mitandao yao ya kijamii Jumatatu waliandika: “Tutacheza dhidi ya mshindi wa pili wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania na FUFA Women Super League (Uganda), Simba Queens FC na Kawempe Muslims Ladies FC mtawalia.”

“Tarehe za safari mbili za Dar es Salaam na Kampala zitajulikana. Mashabiki na wafuasi watasafiri pamoja na timu kwa mechi hizi mbili,” ilisema taarifa hiyo.

Wekundu wa Msimbazi wa Tanzania walimaliza katika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite (SLWPL) wakiwa na pointi 45, pointi moja nyuma ya mabingwa JKT Queens. Timu hiyo ilishinda kombe la ubingwa wa Baraza la Vyama vya Soka vya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kwa Wanawake mwaka 2022. Waliifunga She Corporate FC ya Uganda 1-0 kwenye Uwanja wa Azam mnamo Agosti 27, 2022 na kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa ya Shirikisho la Soka Barani Afrika  (CAF) ya wanawake huko Rabat, Morocco.

Simba ni nyumbani kwa wachezaji wa Kimataifa wa Kenya Corazone Aquino, Ruth Ingotsi, Topister Situma na Jentrix Shikangwa aliyeibuka mfungaji bora wa ligi hiyo kwa kuzititiga nyavu mara 17.

  • Tags

You can share this post!

Wanabodaboda walia abiria wa kike kuwaweka majaribuni...

AMINI USIAMINI: Kipepeo anayefahamika kama ‘glasswing...

T L