• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 7:50 AM
Haaland afunga bao katika mchuano wake wa mwisho kambini mwa Dortmund kabla ya kuhamia Man-City

Haaland afunga bao katika mchuano wake wa mwisho kambini mwa Dortmund kabla ya kuhamia Man-City

Na MASHIRIKA

MSHAMBULIAJI Erling Braut Haaland alifunga bao katika mchuano wake wa mwisho kambini mwa Borussia Dortmund kadri anavyojiandaa sasa kuyoyomea Uingereza kuvalia jezi za Manchester City kuanzia msimu ujao wa 2022-23.

Nyota huyo raia wa Norway alifunga penalti katika ushindi wa 2-1 uliosajiliwa na Dortmund dhidi ya Hertha Berlin katika Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) mnamo Mei 14, 2022.

Kabla ya kipenga cha kuashiria mwanzo wa mechi kupulizwa, sherehe ndogo ya kuaga Haaland iliandaliwa huko mashabiki wakiimba wimbo wa jina la sogora huyo wa zamani wa RB Salzburg.

Haaland ataondoka kambini mwa Dortmund akijivunia kufungia kikosi hicho mabao 86 kutokana na mechi 89 tangu aagane na RB Salzburg mnamo Januari 2020. Haaland aliyefanyiwa na Man-City vipimo vya afya nchini Ubelgiji mnamo Mei 9, 2022, atatua ugani Etihad mnamo Julai baada ya kusajiliwa kwa kima cha Sh7.9 bilioni.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Bei ya mafuta yapanda tena

Kikundi cha wanajuakali Kiambu chafurahia pendekezo la Raila

T L