• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:57 PM
Hoki: Wakenya 2 kusimamia Klabu Bingwa Afrika

Hoki: Wakenya 2 kusimamia Klabu Bingwa Afrika

Na TITUS MAERO

WAKENYA watatu ni miongoni mwa maafisa 22 ambao wameteuliwa na Shirikisho la Magogo Barani Afrika (AfHF) kusimamia makala ya mwaka huu ya mashindano ya Klabu Bingwa Afrika.

Kinyang’anyiro hicho kitang’oa nanga kuanzia Novemba 24 hadi 30, 2021 jijini Accra nchini Ghana.Kupitia kwa taarifa, Afisa wa AfHF Elizabeth King alisema maafisa 22 watasimamia kipute hicho cha haiba kubwa.

Aidha, alieleza kusikitishwa kwa idadi ndogo ya timu ambazo zitashiriki kwenye mashindano hayo zikiwemo timu za kinadada.’Kwa sasa tumepokea uthibitisho wa idadi ndogo ya timu za kinadada na wakati unayoyoma,’ aliongoza.

Maafisa kutoka Kenya wanajumuisha Tina Agunda atakaye kuwa meneja mdogo wa marefa, Peter Mwathe (afisa wa kiufundi) na James Maina (Mpuliza kipenga). Ghana ina idadi kubwa ya maafisa wakiwa 7. Egypt inao 6 na Nigeria ina maafisa 5.Kenya iko na maafisa watatu, huku Namibia ikiwa na afisa mmoja pekee.

Maafisa hao wako na majukumu mbalimbali kwenye pambano hilo.Klabu za midume ni zitakazo shiriki katika shindo hilo ni tisa. niambazo zilijikatia tiketi ya kushiriki katika shindano hilo.Zinajumuisha Eastern Company kutoka Egypt, Zamalek (Egypt), Tairat (Egypt), Army Hockey (Ghana) na Ghana Polisi Service.

Zingine zinajumuisha Ghana Revenue, Wazalendo (Kenya), Kada Stars (Nigeria) na Police Machine (Nigeria).Mabingwa watetezi upande wa midume Egypt Shakia haitashiriki kwenye mashindano hayo.

You can share this post!

Ole Gunar Sokjaer aachishwa kazi

Gor kupiga mechi tatu kujiandalia Caf

T L