• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
Injera atua Fiji kwa mashindano ya McDonald’s Fiji Coral Coast Sevens

Injera atua Fiji kwa mashindano ya McDonald’s Fiji Coral Coast Sevens

NA GEOFFREY ANENE

NYOTA wa timu ya Kenya ya raga ya wachezaji saba kila upande, Collins Injera yuko nchini Fiji kwa ziara ya wiki moja kama balozi wa mashindano ya McDonald’s Fiji Coral Coast Sevens yatakayofanyika Januari 12-14 uwanjani Lawaqa.

Injera, ambaye aliwahi kuwa mfungaji bora wa miguso kwenye Raga za Dunia na kwa sasa anakamata nafasi ya pili kwa miguso 279, nyuma ya Muingereza Dan Norton (358), aliwasili Fiji usiku wa kuamkia Januari 9.

Aliandamana na mke wake Chebet Limo Injera. Watakuwa nchini humo kwa wiki moja. Kama balozi wa mashindano hayo, Injera atakutana na mashabiki wengi wa raga ya Fiji wanaopenda pia raga ya Kenya.

Pia, Injera, ambaye alianzia raga yake katika shule ya upili ya Vihiga Boys, atakuwa mmoja wa maafisa watakaowapa mafunzo watu wanaotaka kucheza raga. Mashindano ya McDonald’s Fiji Coral Coast Sevens yanafanyika kwa mara ya kwanza tangu mkurupuko wa virusi vya corona mwaka 2020.

Hapo kesho, Injera,36, pamoja na nyota wa miaka ya 90 wa raga ya Fiji Sevens Noa Nadruku,55, watatiwa katika orodha ya mashujaa wa mchezo huo (RugbyTown Walk of Fame) wakati wa mashindano hayo.

Majagina walio katika orodha hiyo ni David Campese, Waisale Serevi, Jonah Lomu, Viliame Satala, Ben Gollings, Karl Tenana na Lote Tuqiri.

  • Tags

You can share this post!

BENSON MATHEKA: Hatua za Ruto kumaliza ufisadi zisihujumiwe...

Anayedaiwa kuua wanawe kukaa rumande siku 14

T L