• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 7:50 PM
Inter Milan wapoteza fursa ya kupunguza pengo la alama kati yao na AC Milan ligini

Inter Milan wapoteza fursa ya kupunguza pengo la alama kati yao na AC Milan ligini

Na MASHIRIKA

INTER Milan walipoteza fursa ya kufikia AC Milan kileleni mwa jedwali la Ligi Kuu ya Italia (Serie A) baada ya kuambulia sare tasa dhidi ya Genoa mnamo Ijumaa usiku.

Inter ambao ni mabingwa watetezi wa Serie A walipoteza nafasi nyingi za wazi za kufunga bao katika kipindi cha kwanza kupitia kwa Hakan Calhanoglu. Genoa walikuwa wakiwinda ushindi wa kwanza ligini msimu huu na nusura waupate kupitia kwa Stefano Sturaro mwishoni mwa kipindi cha pili.

Miamba hao kwa sasa wanashikilia nafasi ya pili jedwalini kwa alama 55, mbili nyuma ya viongozi AC Milan walioambulia sare ya 1-1 dhidi ya Udinese katika mchuano mwingine wa Serie A mnamo Ijumaa. Rafael Leao aliwaweka AC Milan kifua mbele kabla ya Destiny Udogie kusawazishia wageni Udinese.

Ilikuwa mara ya tatu katika historia ya Serie A ambapo miamba wawili wa jiji la Milan wamecheza siku ya Ijumaa (isipokuwa wakati ambapo wamekutana wao kwa wao).

Napoli watapaa hadi kileleni mwa jedwali la Serie A kwa alama 57 iwapo watawakomoa Lazio katika mchuano wao wa Jumapili. Wameratibiwa kumenyana na Milan baada ya hapo.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Fainali ya UEFA msimu huu yahamishwa kutoka Urusi hadi...

Joho asema Raila ana timu ya kumfanyia kampeni aingie Ikulu

T L