• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 11:39 AM
Mdogo wa Omanyala kuwakilisha Kenya riadha za Afrika za chipukizi

Mdogo wa Omanyala kuwakilisha Kenya riadha za Afrika za chipukizi

Na GEOFFREY ANENE

KENYA imetaja vikosi vyake vya makala ya nne ya Riadha za Afrika za chipukizi wasiozidi umri wa miaka 18 na miaka 20 zitakazofanyika mjini Lusaka, Zambia mnamo Aprili 29 hadi Mei 3.

Mabingwa wa wa Afrika Mashariki Isaac Omurwa (mbio za mita 100), Jackline Nguyo (100m), Nancy Cherop (3,000m), Samuel Toili (400m), Amos Kipkemoi (800m) na Irine Jepkemboi (kurusha mkuki) ni baadhi ya majina makubwa katika vikosi hivyo.

Omurwa ni ndugu mdogo wa bingwa wa Kip Keino Classic, Afrika na Jumuiya ya Madola Ferdinand Omanyala.

Vikosi hivyo vya jumla ya wanariadha 50 vilichaguliwa baada ya siku mbili ya mashindano ya kitaifa yaliyofanyika ugani Nyayo mjini Nairobi mnamo Aprili 7-8.

Kenya ilikamata nafasi ya pili kwenye makala ya tatu ya Riadha za Afrika U18 na U20 nchini Ivory Coast mwaka 2019 wakati ilizoa medali 17 za dhahabu, 16 za fedha na 11 za shaba.

Kikosi cha Team Kenya U18:

Wasichana

100m: Jackline Nguyo, Sharon Moraa, Selfa Ajiambo; 200m: Sharon Moraa, 800m: Daisy Chepngetich, Dorcas Isoe; 1500m: Janet Chepkemoi, Mary Nyaboke; 2,000m kuruka viunzi na maji: Diana Chepkemoi, Judy Chepkoech; Kurusha mkuki: Christine Musembi; 3,000m: Nancy Cherop, Joyline Chepkemoi

Wavulana 

400m kuruka viunzi: Amos Kipkemei; 200m: Dennis Kiprono; 400m: Samuel Toili; 800m:  Kelvin Kimutai, Phanuel Kipkosgei; 1500m: Joseph Kipkurui, Brian Muange; 2,000m steeplechase: Edmond Serem, Evans Kipkosgei; 3,000m: Andrew Kiptoo, Clinton Kimutai; 10,000m kutembea haraka: Daniel Ekai

Kikosi cha Team Kenya U20

Wanawake

200m: Damaris Nduleve; 400m: Damaris Nduleve; 800m: Everlyne Chepkoech, Judy Kemunto; 1,500m: Peninah Mutisya, Sheila Chebet; 3,000m: Marion Chepngetich, Deborah Chemutai; 3,000m kuruka viunzi na maji: Pamela Kosgei; 5,000m: Diana Cherotich, Maureen Chepkoech; Kurusha mkuki: Irine Jepkemboi

Wanaume

100m: Isaac Omurwa; 200m: Joseph Lenkoima; 800m: Dominic Kiptoo, Brian Kiptum; 1,500m: Gilbert Rono, Ernest Kiprotich, Reynold Kipkorir; 3,000m kuruka viunzi na maji: Solomon Mutisya, Emmanuel Wafula; 5,000m: Vincent Kipruto, Shadrack Rono, Michael Rotich; 10,000m: Amos Kipkurui, Dennis Mutuku, Samuel Kibathi; 10,000m matembezi ya haraka: Stephen Ndangili.

  • Tags

You can share this post!

Aliyejenga kijumba ndani ya nyumba kujificha akiona

Mvua nyingi yafifisha msisimko wa Pasaka

T L