• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 9:01 PM
Jepchirchir ajikwaa wakati wa mbio za New York Mini 10K

Jepchirchir ajikwaa wakati wa mbio za New York Mini 10K

Na GEOFFREY ANENE

BINGWA wa Boston Marathon Peres Jepchirchir amekamilisha mbio za kilomita 10 za New York Mini 10K katika nafasi ya tano Juni 11.

Mkenya huyo, ambaye aliibuka malkia wa mbio za kilomita 42 ya Olimpiki na New York mwaka 2021 na kupigiwa upatu kutawala New York Mini 10K, alitupwa hadi nafasi hiyo baada ya kuanguka alipokanyaga kiatu cha Senbere Teferi.

Muethiopia Teferi, ambaye anashikilia taji la New York Half-Marathon na rekodi ya dunia mbio za kilomita tano, aliishia kutwaa ubingwa wa New York Mini 10K kwa dakika 30:43.

Bingwa wa mbio za mita 10,000 za vyuo vya Amerika, Canada na Puerto Rico (NCAA) Sharon Lokedi kutoka Kenya aliridhika na nafasi ya pili kwa 30:52 naye Mwamerika Keira D’Amato akafunga mduara wa tatu-bora kwa dakika 31:03. Mshindi alizawadiwa Sh1.1 milioni.

Matokeo ya New York Mini 10K (Juni 11):

1. Senbere Teferi dakika 30:43

2. Sharon Lokedi 30:52

3. Keira D’Amato 31:03

4. Aliphine Tuliamuk 31:08

5. Peres Jepchirchir 31:19

6. Viola Cheptoo 31:24

7. Emily Sisson 31:29

8. Caroline Rotich 31:30

9. Sara Hall 31:41

10. Emily Durgin 31:43

  • Tags

You can share this post!

Jaji Mkuu Koome ataka Uhuru atimuliwe kwa kutoteua majaji...

Karua aahidi kuyeyusha umaarufu wa Naibu Rais

T L