• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 10:15 PM
Jezi za Ingwe zanunuliwa kama njugu

Jezi za Ingwe zanunuliwa kama njugu

NA JOHN ASHIHUNDU

JEZI mpya za mashabiki wa AFC Leopards zilizoingia nchini majuzi kutoka Uturuki zinaendelea kununuliwa kama njugu karanga.

Kulingana na Katibu Mkuu wa klabu hiyo kongwe, Gilbert Andugu, Leopards ilinunuwa jezi 3,000, lakini kuna uwezekano wa jezi hizo kumalizika kabla ya msimu mpya kuanza wikendi ijayo.

Jezi hizo zinazobeba nembo ya wadhamini Betika, jezi moja linauzwa kwa Sh2,800 kwa mashabiki waliojiandikisha kama wanachamaa na Sh3,000 wale wasio wanachama.

Kwenye taarifa fupi kutoka kwa klabu hiyo, jezi za watoto zinanunuliwa kwa Sh2,000, huku ikiongeza kwamba malipo yanatumwa kupitia kwa M-PESA pay bill namba 196464 Account number “Replica”.

Betika ndio wadhamini wapya wa Leopards baada ya kuweka saini mkataba wa miaka mitatau wa Sh195 milioni mwezi Julai 2022, kuchukuwa nafasi ya Betsafe waliojiondoa ghafla kwa madai ya uchumi mmbaya.

Andugu alisema, mbali na uwanjani wakati wa mechi zinazuhusu Leopards, jezi hizo kadhalika zinapatiaka kwenye afisi mpya ya klabu hiyo inayopatikana Don Bosco Annex- Matumbato Road, Upper Hill karibu na Kanisa Katoliki la Don Bosco, Nairobi.

Andugu alitoa mwito kwa mashabiki wajitokeze kwa wingi kununua jezi hizo ili pesa wanazolipa ziifaidi klabu kwa njia mbali mbali, huku akiongeza kwamba baadaye jezi za klabu zitaanza kuwafikia mashabiki kupitia kwa afisi katika miji ya Mombasa, Kakamega, Bungoma, Busia, Trans Nzoia, Kisumu, Eldoret, Nyeri na Murang’a.

  • Tags

You can share this post!

Ruto, Raila wang’ang’ania IEBC

Msimu wa Supa Ligi (NSL) kuanza rasmi Novemba 26 kwa mechi...

T L