• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:57 PM
John Terry aacha kazi ya kuwa kocha msaidizi katika kikosi cha Aston Villa

John Terry aacha kazi ya kuwa kocha msaidizi katika kikosi cha Aston Villa

Na MASHIRIKA

ALIYEKUWA beki na nahodha wa Chelsea, John Terry, 40, ameacha kazi ya kuwa kocha msaidizi kambini mwa Aston Villa ili kuzamia mafunzo zaidi yatakayomshuhudia akiwa mkufunzi mkuu wa timu yoyote katika siku za usoni.

Nyota huyo raia wa Uingereza alijiunga na benchi ya kiufundi ya Villa inayosimamiwa na mkufunzi Dean Smith mnamo Oktoba 2018.

Alisaidia Villa kupandishwa ngazi kutoka Ligi ya Daraja la Kwanza (Championship) hadi Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) mnamo 2019.

Terry aliwahi kuhusishwa na nafasi za ukufunzi kambini mwa Bournemouth na Celtic mnamo Februari 2021 kabla ya vikosi hivyo kupata makocha wapya.

Baada ya kukwezwa daraja hadi EPL, Villa walitinga fainali ya Carabao Cup mnamo 2019-20. Kikosi hicho kiliponea chupuchupu kuteremshwa daraja kwenye EPL mnamo 2019-20 kabla ya kuambulia nafasi ya 11 mnamo 2021-22.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Barcelona, Juventus na Real Madrid waendelea kutetea...

Fowadi Erik Lamela ayoyomea Sevilla