• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 2:32 PM
Fowadi Erik Lamela ayoyomea Sevilla

Fowadi Erik Lamela ayoyomea Sevilla

Na MASHIRIKA

TOTTENHAM Hotspur wamemsajili fowadi Bryan Gil wa Sevilla kwa Sh3.9 bilioni huku kiungo Erik Lamela akijiunga na miamba hao wa Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga) kama sehemu ya dili hiyo ya uhamisho.

Gil, 22, ambaye amekubali kutia saini mkataba wa miaka mitano, alichezea Uhispania kwa mara ya kwanza mnamo Machi na kwa sasa ni sehemu ya kikosi kinachoshiriki Olimpiki za Tokyo, Japan.

Sogora huyo aliwajibishwa na Sevilla kwenye La Liga mara 14 mnamo 2020-21 na alitokea benchi katika mashindano yote.

Lamela ambaye ni raia wa Argentina mwenye umri wa miaka 29, alijiunga na Spurs mnamo 2013 kwa kima cha Sh4 bilioni.

Lamela ni miongoni mwa wachezaji saba wakiwemo Christian Eriksen, Roberto Soldado, Paulinho, Etienne Capoue, Vlad Chiriches na Nacer Chadli ambao Spurs walisajili mnamo 2013 baada ya Gareth Bale kujiunga na Real Madrid ya Uhispania kwa Sh13 bilioni.

Lamela alifungia Spurs mabao 37 katika mechi 255 na alikuwa miongoni mwa wachezaji wa akiba katika fainali iliyowashuhudia wakipigwa na Liverpool mnamo 2019.

Gil alipokezwa malezi wa soka katika akademia ya Sevilla kabla ya kuunga kikosi cha watu wazima kwa mara ya kwanza mnamo Januari 2019. Alichezea kikosi hicho kwa mara ya mwisho mnamo Septemba 2020 kabla ya kujiunga na Eibar kwa mkopo.

Alipachika wavuni mabao manne katika mechi 28 za La Liga mnamo 2020-21 ambapo Eibar walikokota nanga mkiani mwa jedwali la Ligi Kuu.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

John Terry aacha kazi ya kuwa kocha msaidizi katika kikosi...

Serikali yakiri kudaiwa Sh16m za usalama wa baharini