• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:57 PM
Karan Patel na Jasmeet Chana wanafufua uadui Nanyuki Rally

Karan Patel na Jasmeet Chana wanafufua uadui Nanyuki Rally

Na GEOFFREY ANENE

KIVUMBI kinatarajiwa wakati madereva 21 watawania pointi kwenye duru ya sita ya Mbio za Magari za Kitaifa Kenya (KNRC) Nanyuki Rally mnamo Jumamosi.

Vita vinatarajiwa kuwa vikali zaidi juu ya jedwali ambako kiongozi Karan Patel na nambari mbili Jasmeet Chana watawinda kuonyeshana ubabe wakipaisha magari ya Mitsubishi Evolution 10. Karan ana pointi 135 naye Jasmeet yuko alama moja nyuma.

Makinda Hamza Anwar, Maxine Wahome na Jeremiah Wahome, ambao wanakuzwa na mradi wa kukuzwa na Shirikisho la Kimataifa la Mbio za Magari (FIA) kuwa nyota wa baadaye, pia wako katika orodha ya washiriki.

Dereva mzee katika duru hii ni Frank Tundo aliye na umri wa miaka 73 naye mchanga ni Rio Smith (20).

Bingwa wa Afrika 2021 Carl Tundo,48, ambaye ni mwanawe Frank, atakuwa akishiriki duru yake ya pili ya KNRC mwaka huu baada ya ile ya dunia ya Safari Rally mwezi Juni. Carl atatumia mwelekezi mpya Sam Taylor baada ya Tim Jessop kubanwa na shughuli nyingi.

Nanyuki Rally inajumuisha kilomita 153 za kuwania pointi. Itafanyika katika maeneo ya Mlima Hema, Greystones na Ole Naishu.

Karan Patel anaongoza jedwali baada ya duru tano za kwanza kwa alama 135 akifuatiwa na Jasmeet Chana (134), Kush Patel (54), Leo Varese (51), Maxine Wahome (46), Jeremiah Wahome (41), Ghalib Hajee (40), Carl Tundo (39), Steve Mwangi (36) na Zameer Verjee (33).

Orodha ya washiriki wa KCB Nanyuki Rally:

1 #16 Raaji Singh Bharij/Ravi Soni (Skoda Fabia -R5)

2 #12 Hamza Anwar/Adnan Din (Mitsubishi Evolution 10)

3 #6 Jasmeet Chana/Ravi Chana (Mitsubishi Evolution 10)

4 #3 Karan Karan K Patel/Tauseef Khan (Mitsubishi Evolution 10)

5 #10 Piero Cannobio/Fabrizia Pons (Hyundai-R5)

6 #19 Nikhil Sachania/Deep Patel (Mitsubishi Evolution 10)

7 #23 Steve Mwangi/Dennis Mwenda (Subaru Impreza)

8 #18 Issa Amwari/Edward Njorog (Mitsubishi Evolution 10)

9 #1 Carl Flash Tundo/Samuel Taylor (Triumph TR 7-Classic)

10 #9 Ian Duncan/Jaspal Matharu (Nissan Datsun-Classic)

11 #51 Piers Daykin/Tariq Malik (Datsun 280 Z-Classic)

12 #50 Frank Tundo/Gareth Dawe (Ford Fiesta Proto – SPV)

13 #20 Maxine Wahome/Murage Waigwa (Subaru Impreza)

14 #22 Kush Patel/Mudasar Chaudry (Subaru Impreza – S)

15 #34 Shakeel Khan/Assad Mughal (Ford Escort -Classic)

16 #35 Rajveer Thethy/Wayne Fernande (Subaru Impreza)

17 Rio Smith/Riyaz Ismail (Ford Fiesta-2WD)

18 #32 Edward Maina/Anthony Gichohi (Subaru Impreza -S)

19 #29 Daren Miranda/Vinay Varsani (Subaru Impreza -2WD)

20 #44 Leo Leonardo Varese/Kigo Kareithi (Toyota Auris -2WD)

21 #43 Sameer Nanji/Vinay Shah (VW Golf MK2 -2WD)

  • Tags

You can share this post!

Nassir akabiliwa na changamoto tele katika kutatua suala la...

100 wafa, maelfu wapoteza makao katika janga la mafuriko...

T L