• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 9:50 AM
Kaunti ya Kakamega yakarabati viwanja kuanzia mashinani

Kaunti ya Kakamega yakarabati viwanja kuanzia mashinani

Na JOHN ASHIHUNDU

SERIKALI ya Kaunti ya Kakamega imeanza kukarabati viwanja kwa michezo kuanzia mashinani katika juhudi za kuimarisha michezo na kukuza vipaji miongoni mwa vijana.

Akizungmza wakati wa fainali za Kombe la Governor’s Cup kwa timu za Wadi ya Isukha Kusini, Rachel Atamba ambaye ni Waziri wa Biashara, Viwanda na Utalii katika Kaunti ya Kakamega alisema Serikali ya Gavana Fernandes Barasa itahakikisha kila eneobunge litakuwa na angalau uwanja mmoja wa kisasa.

Waziri wa Biashara, Viwanda na Utalii katika Kaunti ya Kakamega Bi Rachel Atamba (kushoto). PICHA | JOHN ASHIHUNDU

Kakamega ina maeneobunge 12 ambayo ni Shinyalu, Navakholo, Mumias Mashariki, Mumias Magharibi, Matungu, Malava, Lurambi, Likuyani, Khwisero, Ikolomani, na Butere.

Diwani (MCA) wa Isukha Kusini Charles Lwanga aliyehudhuria fainali Wadi yake kati ya Titanic FC na Mukumu Lyon alisema hatua hiyo itaimarisha vipaji miongoni mwa vijana katika kaunti hiyo inayofahamika kwa kutoa wanasoka wengi waliochezea klabu kubwa na Harambee Stars.

Atamba aliyeandamana na Afisa Mkuu wa Michezo katika kaunti hiyo, Joseph Alucheri, alisema gavana Basara ameonyesha mapenzi yake kwa kujitolea kudhamini mashindano mbalimbali tangu 2020.

Alisema atahakikisha mipango yoyote ya kuimarisha michezo katika kaunti hiyo imetiliwa mkazo kwa ajili ya kupunguza uhalifu miongoni mwa vijana wasio na kazi.

Wakati wa fainali hiyo iliyovutia mashabiki wengi wakiwemo wanasoka wa zamani Washington Muhanji na Tony Lidonde, timu ya Titanic inayonolewa na Davies Ingoi Imbayi iliichapa Mukumu Lyon 1-0 na kufuzu kwa fainali tarafa ya Shinyalu.

Museno Sambakhalu ilimaliza katika nafasi ya tatu baada ya kuibwaga Mundulu FC 2-1 katika mechi ya kuwania nafasi ya tatu na nne.

Alucheri alisema wachezaji watakaoteuliwa watapata ufadhili wa masomo ya juu kutoka kwa Chuo Kikuu cha Zetech, hii ikiwa mara ya tatu tangu mashindano hayo yaanza miaka mitatu iliyopita.

  • Tags

You can share this post!

Pasta Ng’ang’a afokea serikali kuhusu ushuru wa juu

Nilisema Omosh alikaa muigizaji wa video ya harusi mkadhani...

T L