• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 7:50 AM
KBC kupeperusha Safari Rally, imesaini kandarasi na WRC ya Sh50 milioni

KBC kupeperusha Safari Rally, imesaini kandarasi na WRC ya Sh50 milioni

Na PETER NJENGA

SHIRIKA la Utangazaji la Kenya (KBC) litapeperushia mashabiki wa Mbio za Magari za Dunia za Safari Rally mnamo Juni 24-27 baada ya kupata haki za kufanya hivyo kwa kusaini kandarasi ya Sh50 milioni Jumatatu.

Katika mpango huo, shirika hilo litapata picha na video kutoka kwa washikilizi wa haki za kibiashara za WRC kupitia runinga yao ya WRC+.

KBC itashughulika pia na madereva wa humu nchini ambao huenda wasionyeshwe kwenye runinga ya kimataifa wakati wa mbio hizo zitakazofanyika katika kaunti za Nairobi na Kiambu na eneobunge la Naivasha katika kaunti ya Nakuru.

Safari Rally, ambayo inarejea kwenye WRC baada ya miaka 19, inatarajiwa kuvutia zaidi ya watazamaji 70 milioni kwenye runinga kutoka mataifa 150. Isitoshe, mashabiki zaidi wanatarajiwa katika eneo la Naivasha, ambalo litaandaa asilimia kubwa ya Safari Rally, mara tu serikali italegeza ama kuondoa marufuku dhidi ya mikusanyiko mikubwa ya wanamichezo.

Marufuku hiyo imekuwa tangu mkurupuko wa virusi vya corona mwezi Machi 2020. Virusi hivyo vimeua watu 3,308 humu nchini. Maambukizi 172, 639 ya virusi hivyo hatari yalikuwa yameripotiwa nchini Kenya kufikia Juni 7.

  • Tags

You can share this post!

Amerika yapepeta Mexico kwenye fainali ya Concacaf Nations...

Moraa atesa mbio za mita 800 nchini Finland kinadada...